Usiwategemee Watu – part 3

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Usiwategemee Watu – part 3
Loading
/
Mwanzo 4:13-15

Hujambo na karibu. Leo twapata somo letu kutoka Mwanzo 4:13-15. Usiwategemee watu. Hiki ni kipindi cha matumaini, jina langu ni David Mungai. msikilizaji nakuambia wazi ya kwamba ni ghari mno kuishi maisha ya kujipenda na Zaidi maisha ya kujipenda kupita kiasi, huleta maangamizi. Usiwategemee watu saana. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba, mzaliwa wa kwanza duniani hii, alileta chuki, na ukaidi. Na tunaona vile Mungu huwatendea wanaowachukia wengine na kuwadharao. Biblia yatuonyesha wazi vile Mungu huwahukumu wanaomwasi na kumkaidi, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mwanzo 4:13-15


“Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa naichukuliki. Tazama umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, name nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani, hata itakuwa kila anionaye ataniua. Bwana akamwambia, kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.”

Kutoka kwa fungu hilo, twaweza kupata mawaidha kadhaa yenye msaada maishani. Kaini ampa Mungu changamoto. “Bwana adhabu yangu imenikulia kubwa haichukuliki” kaini aona adhabu kubwa lakini hakumbuki alimwua ndugu yake aliyeitwa nabii. Anasema kwamba adhabu yake ni kubwa. Anaona kana kwamba Mungu hafanyi haki. Halafu akasema “Tazama umenifukuza leo katika uso wa ardhi nitasitirika mbali na uso wako, name nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani hata itakuwa kila anionaye ataniua” Mwenyewe aliamua kumwua ndugu yake. Sasa anateta kwamba hukumu ni ngumu, wala haombi msamaha na kutubu dhambi zake. Kiburi na majivuno kaini anajipenda sana na kwa sababu hiyo Mungu akatoa hukumu yake bila huruma. Utaishi kama mtoro. Hakuna mahali pa kupumzika; kama vile mtu mmoja amesema. “ Afadhali kupumzika katika kaburi kuliko kuishi bila mapumziko.” Kama ni kutembea ni kutembea tu bila kusimama, bila kuketibila usingizi ungependa kumpumzika kaburini lakini kifo cha kukataa. Hii ndiyo sababu Mungu alisema
“Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia kaini alama. Mtu amwonaye asije akampiga.”

Kaini aliishi na hukumu yake, lakini hakuna mtu atakuua. Mtu akikuua talipiza mara saba. Hautaweza kuondokea au kutoroka kutoka kwa hiyo dhambi na Mungu akamweka alama. Kaini asiuawe, aishi na dhambi yake. Na hukumu ya Mungu ikawa ndiyo mwisho bila swali au maswali. Mungu ndiye hujua yaliyo haki, hakuna mabishano. Na ni yeye tu wakutegemewa. Mwanadamu hakupeleki popote. Kama siyo kiburi na majivuno yake kaini angalitubu asemehewe dhambi zake. Kiburi huja kabla kuanguka. Acha kiburi msikilizaji tubu na utasamehewa dhambi zako. Mungu ni wa huruma nyingi. Na ni wa kutegemewa. Mtume Petro atushauri hivi: 1 Petro 5:6
“Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari ili awakweze kwa wakati wake. Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote. Kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!