Usiwategemee Watu – part 1

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Usiwategemee Watu – part 1
Loading
/
Mwanzo 4:8

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini twalichambua Neno kutoka Mwanzo 4:8. Naitwa David Mungai. katika kitabu cha Mwanzo 4:8 twapata habari ya ndugu wawili kaini na Habili, na tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa ndugu hao wawili. Nasoma sasa kutoka Mwanzo 4:8

“Kaini akamwambia Habili nduguye, twende uwandani. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye akamuua.”

Ni neno la kuhuzunisha kweli. Kaini kamuua ndugu yake Habili. Kuua ni dhambi; dhambi ya unafiki n ahata wivu. Kaini akamwokea ndugu yake mtega. Alijianya kana kwamba ni matembezi ya kawaida, kumbe alikusudia maovu. Neno limesema katika mstari wa 8:

“Kaini akamwambia Habili nduguye (Twende uwandani) ikawa walipokuwapo uwandani kaini akamwinukia Habili nduguye akamuua.”

Hatujui Kaini alitumia silaha gani kumuua ndugu yake, lakini ukweli ni kwamba alimuua ndugu yake. Ni dhambi aliyokusudia aliyopanga kutenda, na alikuwa tayari kumchinja ndugu yake kama vitani. Kwa kigiriki ni kumchinja mtu kama ngombe au mbuzi. Hivyo sababa sadaka yake ilikataliwa na Mungu, ya Habili ikakubaliw. Kaini akakasirika akagadhabika, ili aondoe hiyo hasira, akaona amuue ndugu yake Kaini, si mtu wa kutegemewa, na si mtu wa kuaminika. Ikawa ni kinyume cha mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Kaini akawa mfano mwovu wa kuigwa. Huwezi kumfuata kaini, maana si wa kutegemewa. Pamoja na hayo, kifo cha Habili hakikutarajiwa. Alimwamini ndugu yake. Hakuonywa na mtu na hukudhania kwamba ndugu yake angemfanya hivyo wala hakujua angeishi kwa miaka mingapi. Alilojua ni kwamba yeye ni mwanadamu na siku moja atakufa, lakini hakutarajia kufa haraka vile. Hata wewe name hatujui tutaingia hii dunia hata lini. Hata hivyo alijua siku moja atakufa maana Mungu alikuwa amemwambia Adamu.

“Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usite, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile kwa maana siku utakapokula matunda ya mtu huo utakufa hakika.”

Habili kweli hakurajia kufa upesi na haraka vile. Msikilizaji kweli twajua ya kwamba Yesu Kristo asiporudi upesi tutakufa lakini hiyo ni siri ya mwenyezi Mungu. Habili kwa sababu alikuwa mtu adilifu mwenye haki mbele zake mungu, sadaka yake ilikubaliwa na mwenyezi na alipouawa akaaga dunia, alikaribishwa mbinguni. Alikufa kwa sababu ya Imani yake, kifo cha watakatifu. Tujitayarishe kama Habili tuwe na uhusiano mwema na Mwenyezi Mungu. Usimtegemee mtu bali mtegemee na ujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu, katika Kristo Yesu na ujitoe kama dhabihu takatifu tena iliyo hai kwake Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!