Akili Ni Nywele

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Akili Ni Nywele
Loading
/
Mwanzo 41:1-13

Hujambo na karibu. Jina langu ni David Mungai na ni furaha yetu kukuletea matumaini kipindi cha kulichambua neno la mungu. Leo twalitazama neno kutoka Mwanzo 41:1-3. Akili ni nywele. Naam, wahenga wetu wa zamani walisema “Akili ni nywele kila mtu ana zake” lakini twapaswa kuwajibika vizuri kwa namna tunavyozitumikisha akili zetu na Zaidi twapaswa kuzikuza. Mambo mawili, 1. Namna ya kuzitumikisha akili zetu na kuzikuza.”

Mungu huwasiliana nasi kwa akili zetu nasi pia huzitumia akili hizo hizo kuwasiliana kila mmoja na mwingine. Mungu huwasiliana na akili mbalimbai na kwa njia kadhaa. Nasoma sasa kutoka kitabu cha Mwanzo 41:1-13.

“Ikawa mwisho wa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto, na tazama amesimama kando yam to. Na tazama ngombe saba wazuri wanono walipanda kutoka mtoni wakajilisha manyasini. Na tazama ngombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya wamekonda wakasimama karibu na wale ngombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ngombe wabaya waliondoka wakawala wale ngombe saba wazuri, wanono. Basi farao akaamka, akalala akaota ndoto mara ya pili. Tazama masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa mema. Na tazama masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi farao akaamka, kumbe ni ndoto tu.

Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, nayakumbuka makossa yangu leo. Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwa nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji. Tukaota ndoto usiku mmoja mimi nay eye. Kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake tukaota. Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatutafsiria ndoto zetu, akamtafasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. Ikawa kama vile aliyotufasiria ndivyo ilivyotokea; mimi nalirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa.”

Fungu hili la neno la mungu laonyesha kweli mungu anaweza kutumia akili zetu apate kuwasiliana nasi. Hatujui Farao alikuwa akifanya nini wakati wa mchana kabla ya kulala usiku.

Nasema hivyo, maana kuna watu wanaota kulingana nay ale alikuwa akifanya mchana. Kwa mfano, kama ni mwanafunzi wa hesabu. Kunao wakati hulala usiku mzima akiota ndoto za kufanya hesabu. Hatujui farao alikuwa akifanya nini wakati wa mchana lakini aliota. Ndoto, katika ndoto aliona ngombe saba wakonde na wengine saba wanono. Wakonde wakawala wale wanono.

Tafsiri likawa kwamba nchi ya misri itakuwa na miaka saba ya njaa na miaka saba ya shibe. Ukwlei na tafsiri zikapatikana. Akili za waganga zilipeana habari pia. Farao alikuwa na huzuni na ugumu wa moyo, wachawi waliposhindwa kutafsiri, na farao akaachwa bila kujua mbele wa nyuma. Pia kulikuwa akili za yule mnyweshaji na akili zake zilizaa mazao mema. Alimwambia farao vile kijana. Mwebrania yusufu alivyomsaidia wakiwa. Gerezani namna ya kuitafsiri ndoto yake Yusufu alivyomsaidia wakiwa gerezani namna ya kuitafsiri ndoto yake Yusufu akaletwa na akamtafsiria ndoto yake yusufu akaletwa na akamtafisria ndoto. Akili za mnyweshaji hazikusahau, Yusufu walipokuwa pamoja gerezani. Siyo mambo yote yanayomtoka mtu akilini hasa yale mem ahata, maovu uliyotenda awali.

Hapa pia twaona, vile mungu alitimiza upendo wake Yusufu maana miaka miwili iliyopita yusufu alikuwa analia apelekwe kwa farao akajitetea na kumwonyesha ya kwamba haikuwa haki kuwekwa gerezani maana ukweli ni kwamba hakutaka kulala na mke wa mwajiri wake potifa.Mungu akatumia akili za munyeshaji kutimiz mapenzi ya Yusufi. Mungu aliita tutumie akili zetu kwa hekima na kwa njia za kujenga wala si kubomoa. Neno lasema, warumi 12:1-2 “Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza mungu ndiyo ibada yenu yenye maana bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu”

Twaziweka nia/akili zetu upya kwa kulisoma, kulitafakari neno la mungu, pia tumruhusu roho mtakatifu aishi ndani ya mioyo yetu, kwa kutubu na kuingama dhambi zetu, na kuacha njia za dhambi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!