Je Mungu Anaweza Kuleta Mabadiliko

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Je Mungu Anaweza Kuleta Mabadiliko
/
Mwanzo 38:1-6

Hujambo na karibu katika kipindi hiki cha matumaini. Leo twajiuliza swali hili. “Je, mungu anaweza kuleta mabadiliko?” Jina langu ni David Mungai. Tuanze kujiuliza swali hili, Je, dini zote ziko sawa? Hapana, dini zote si sawa kwa sababu, kwa mfano. Mungu katika dini ya waisraeli ilibidi wapewe amri kumi mlimani Sinai. Katika dini ya ukristo ilimbidi mungu kumtoa yesu kristo afe msalabani kila anayemwamini apate kuwa mkristo. Yalikuwa mapenzi ya mungu kuwasiliana nasi, katika kristo. Na hii ndiyo tofauti kubwa iliopo kati ya dini zingine na uksristo.

Katika dini zingine watu, humtolea kafara kuwatafuta miungu yao lakini katika ukristo mungu hunitafuta mwanadamu kwa kristo kushuka kutoka mbinguni hadi hapa duniani. Na katika ukristo, uhusiano wetu na mungu hupatikana kwa kumwamini yesu kristo na ni uhusiano wa kudumu.

Tangu zamani, mungu alijitoa kumwumba adamu kusudi na mathumuni yake ni kuwa na uhusiano mwema na mtu aliyeumba. Nuhu alitengeneza safina kufuatana na maelekezo yake mungu ili hatimaye yeye n afamilia yake wapate kuokolewa na maafa ya gharika. Abrahamu aliteuliwa na mungu kutoka kwa mataifa kusudi wekwe na mungu katika nchi ya ahadi.

Katika ujumbe wetu wa leo twajifunza na kuona vile ndugu zake walimuuza kama mtumwa lakini hatimaye yusufu akawa msaada kwa familia ya yakobo walipokubwa na janga la njaa. Walipomuuza yusufu alikuwa mvulana mdogo, kati ya miaka 17 na 18 ya umri. Je, sasa, kwa sababu ameuzwa kama mtumwa kwa washmaeli, Je, mungu ataleta mabadiliko? Nasoma kutoka kitabu cha Mwanzo 39:1-6

“Basi yusufu akaletwa mpaka misri naye potifa akida wa farao mkuu wa skari mtu wa misri akamnunua mkononi mwa hao waishmaeli waliomleta huko. Bwana akawa pamoja na yusufu, naye akastawi naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule mmisiri. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye nay a kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake. Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake na vyote vilivyomo Bwana akabariki nyumba ya yule mmisri kwa ajili ya yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba na katika shamba. Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa yusufu wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.”

Swali Je mungu huleta mabadiliko? Hapa twapata vitendo kadhaa alivyofanya potifa na twaona vile mungu alileta mabadiliko maishani mwa yusufu. Mungu akamtumia mtu wa kabila n ahata taifa linguine. Kuleta mabadiliko maishani mwa yusufu. Tuache ubaguzi. Jambo la kwanza. Potifa alimnunua yusufu kutoka kwa waishmaeli. Hatujui alimnunua kwa pesa ngapi; yote tunayojua ni kwamba alipokuwa nyumbani mwa potifa; potifa alimfunza yusufu mambo mengi. Pamoja na hayo tumesoma ya kwamba “mungu alikuwa pamoja na yusufu, na mungu akamfanikisha. Anayemcha mungu; mungu mwenyewe humfanikisha.”

Jambo la pili. Polita aliona ya kwamba, mungu alikuwa pamoja na yusufu, mungu wa Israeli alikuwa naye. Na mungu wa Israeli ni mungu aliye tofauti na miungu wengine; na kwa sababu hiyo potifa akampandisha yusufu cheo, akampa mamlaka Zaidi. Msikilizaji uwepo wa mungu ukiwa pamoja nawe na uwe ndani yako mungu atajidhihirisha kwako na madaraka utapata kwa wakati unaofaa. Jambo la tatu. Potifa alimwamini yusufu. Neno lasema “ikawa tokea wakati alipomweka awe asimamizi juu ya nyumba nan yote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule mmisri kwa ajili ya yusufu. Mbaraka wa Bwana ikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba na katika shamba.”

Yusufu akapewa mamlaka ya nje na ndani. Ukweli ni kwamba uaminifu katika huduma huleta faida kwa utukufu wake mungu. Waliomuuza yusufu hawakuondoa uwepo wa mungu maishani mwake. Watu watakuzingizia lakini ukibaki mwaminifu kwake mungu hatakuacha wala kupungukiwa kamwe. La sivyo mungu hatakuwa mungu kwako. Mungu huleta mabadiliko kwa wale wanaomcha mungu. Tmtukuze mwokozi yesu kristo maana kama vile neno limesema. Mungu hatatuacha wala kutupungukia. Heri anayemcha mungu.