Mungu na ulimwengu wa uovu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu na ulimwengu wa uovu
Loading
/
Mwanzo 6:8-13

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha kulichambuaneno la Mungu matumaini. Leo, twalitazama Neno kutoka Mwanzo 6:8-13 Mungu na ulimwengu wa uovu. Jina langu ni David Mungai.

Mungu na ulimwengu wa uovu maana yake nini? Kila mmoja angeona heri kama tungalikuwa namajibu ya kila swali. Lakini nasikitika kwa akili zetu haiwezekani. Neon la Mungu latufunza ya kwamba tangu jadi ulimwengu umejawa na maovu. Katika Mwanzo 6:8-13, twapata habari ya vile Mungu alitoabhukumu ulimwenguni kwa sababu ya uovu wa mwanadamu. Nasoma sasa kutoka Mwanzo 6:8-13

Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana. Hivi ndivyo vizaizi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki mkamilifu katika vizazi vyake, Nuhu alikwenda pamoja na Mungu. Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu na Hamu na Yafethi. Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. Mungu akaiona dunia na tazama imeharibika maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mungu akawambambia Nuhu, wmisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu, kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.

Fungu hili la Neno la Mungu latupa mambo kadhaa yenye msaada kwetu. Mungu alisema na nuhu kwa sabbau alikuwa mnyenyekevu. Kiburi na majivuno hayakuonekana kwake. Neno lasema. Mstari wa nane. Mwanzo 6:8 “Nuhu akapata neema machoni pa Bwana” Kwa sababu Mungu hupendezwa na watu wanyenyekevu. Na unyenyekevu kumwelekeza mtu katika maisha adilifu. Na hii ndiyo kiburi huleta kuanguka kwa mtu, maana Mungu humpinga mwenye kiburi. Zaidi twaona ya kwamba Nuhu aliwatendea watu wengine haki. Mstari wa 9 “Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikwa mtu wa haki mkamilifu katika vizazi vyake..Nuhu alikwenda na Mungu..”

Nuhu alikuwa na ushirika mwema na Mungu. Ingawaje Nuhu alizirwa na maovu, alisimama wima na aksiahi kwa Amani na Mungu na wanadamu wenzake. Zaidi sana alikuwa mvumilivu na mvumilivu hula mbivu. Naomba kwamba hata nasi tuwe wanyekevu mbele zake Mungu ili tuueneze wema wa Mwenyezi Mungu. Maneno ya mstari wa 11, yasema kwamba dunia ilijaa dhuluma na uovu kila mahali, na mioyo ya watu haikukoma kuwa mbovu, na waliendelea kuwa maovu. Ufisadi wa akili na huonekana katika matendo na mienendo yetu. Jambo la kushtusha mtu, maana hukumu yaja, tena upesi. Mungu akajua ni nini kilikuwa kinaendelea. Alitazama na akaona.

Mungu huona na kusikia- Ni Mungu aliye hai na ataishi milele na milele amina. Hata hivyo, sharti na lazima tujue ya kwamba hukumu yaja. Kila goti litapigwa mbele ya kiti cha enzi cha Mwenezi Mungu. Na kila mtu atahukumiwa, yeye mwenyewe binafsi. Sasa tukiwa katika ya kusubiri hiyo siku ya hukumu; huruma zake Mungu ni nyingi tukitubu Yeye hutusamehe na kuhuisha kufufufa tumaini letu za uzima wa milele.

Maovu ni mengi lakini usisahau ya kwmaba \mungu wetu ni wa huruma katika Yesu Kristo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!