Thamani Ya Shida

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Thamani Ya Shida
Loading
/
Mwanzo 37:1-11

Hujambo. Naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea matumaini. Hik ni kipindi cha kulichambua somo letu kutoka kitabu cha Mwanzo 37:1-11. Ni jambo la kustajabisha kusema ya kuwa mna thamani katika shida. Sisi hufikiria ya kwamba mna thamani katika mambo mazuri tu. Hauwezi kuweka thamani kwa viazi vilivyooza, lakini kwa mkulima, viazi vilivyooza ni mbolea.

Maishani pia hatuwezi kufikia thamani ya kitu Fulani kwa kufikiria tu. Kupata thamani ya kitu Fulani lazima ufikirie kwanza. Hebu nisome neno kutoka kitabu cha Mwanzo 37:1-11

Yakobo akakaa katika nchi aliyosafiri baba yake, katika nchi ya kanaani. Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na wana wa Bilha na wana wa Zilipa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya. Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia wala hawakuweza kusema naye kwa Amani. Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia. Akawaambia tafadhalini; sikieni ndoto hii niliyoiota, tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka, ikainama mbele ya mganda wangu.

Ndugu zake wakamwambia; Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Akaota tena ndoto nyingine akawaambia ndugu zake, akasema, angalieni nimeota nyingine, na tazama jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawaambia baba yake na ndugu zake, baba yake akamkemea akamwambia, ni ndoto gani hii uliyoita? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu. Bali baba yake akalihifidhi neno hili.

Hali ya nyumbani kwake Yakobo yatuonyesha namna ya kuweka thamani katika jambo. Msikilizaji, kulingana na tunavyosoma kutoka kitabu hiki cha Biblia, twamsoma Yakobo na vile aliishi kwa mjomba wake Labani kwa miaka ishirini. Alifanya kazi ya uchungaji wa kondoo. Yakobo alikuwa bado kijana alipozungumza na Labani, wakakubaliana kwamba, Yakobo atafanya kazi miaka saba ili aruhusiwe kumuoa Raheli, lakini siku ya kumchukua Raheli awe mke, alipewa Leah, aliyekuwa dada yake mkubwa. Yakobo hakumpenda Leah kwa sababu alikuwa na macho mabaya. Bila kujua akapewa Leah. Asubuhi aliona ya kwamba Labani alimkosea alipouliza aliambiwa kwamba mira yao haukumruhusu binti wa pili kuolewa kabla wa kwanza. Basi Yakobo akaambiwa ya kwamba iwapo bado alimpenda Raheli ilibidi afanye kazi kwa Labani miaka saba. Akafanya hivyo.

Sasa hapa katika surah ii ya mwanzo 37:1-11, Yakobo ni mzee na wanawe ni wanaume wazima na walizaliwa na mke wake wa kwanza leah.

Kwa miaka mingi raheli alikaa tasa, lakini katika siku za uzeeni alijifungua kijana mwanaume jina lake Yusufu. Yakobo akampenda sana kumliko mwanawe wa kwanza reubeni. Yakobo akamshonea yusufu nguo safi kuliko za wana wengine. Akaonyesha mapendeleo. Mbona hakuwatendea na wengine vile. Yusufu naye alianza kuota ndoto zilizoonyesha ya kuwa kuna uwezekano kwamba atawatawala.

Biblia imetuonyesha wazi ya kuwa Yusufu baadaye aliuzwa kama mtumwa akapelekwa misri na hatimae akawa na mamlaka makuu katika nchi ya msiri na hatimaye ndugu zake na wote katika familia walimwemdea Yusufu kwa msaada wa chakula. Twaona ya kwmaba kweli Mungu alikuwa katika jambo hili, maana mateso yake Yusufu yaligeuka kuwa msaada kw awatu wa familia yake. Sababu ni kwamba, Yusufu alimhusisha Mungu katika kutenda mema kwa ndugu zake. Hakutafuta kulipisha kisasi, kwa sababu alimhusisha Mungu na alitafuta kufanya mapenzi yake Mungu. Msikilizaji ukitamani thamani ya kujenga siyo ya kubomoa, mhushishe Mungu kama linavyosema Neno lake.

Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake” msikilizaji heri wewe umapomkabidhi mungu fadhaa zako zote.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!