Usemi Wa Lugha

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Usemi Wa Lugha
Loading
/
I Wakorintho 14:10-32

Natumai u buheri wa afya msikilizaji wangu. Karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua fungu la neno kutoka 1 Wakorintho 14:10-22 ‘Usemi wa Lugha’. Jina langu ni David Mungai, burudika kwa wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena; twalichambua fungu la neno 1 Wakorintho 14:10-22 Usemaji wa lugha.

Twashangaa lugha zilitoka wapi? Baadhi ya wasomi husema kwamba tuliumbwa kutoka kwa wanyama, na wanaendelea kusema ya kwamba lugha zilitokana kwa kurudia maneno machache na hatimaye tukapata lugha. Lakini Biblia yatoa ukweli kwamba Adamu, alikuwa na umaarufu wa lugha, maana aliweza kuwapa majina wanyama wote.

Pia twajua ya kwamba, Mungu alitumia maneno Kuumba vitu vyote. Katika kitabu cha Mwanzo 11:6-9 twapata maneno haya…

6 Bwana akasema, tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja, na haya Ndiyo wanayoanza, wala hawatazuiliwa neno wanaokusudia kulifanya.

7 Haya, natushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote wakaacha kuujenga ule mji.

9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli, maana hapo ndipo Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”

Mungu alijifunua kwetu, Mwanzo kwa lugha ya kiebrania na kigiriki au kuyunani- lugha za Biblia.

Katika fungu la neno linalopatikana katika 1 Wakorintho 14, Paulo ajaribu kutueleza shida ya Lugha katika mwili wa Kristo- Kausa. Nasoma. 1 Wakorintho 14:10-22.

10 “ Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani wala hakuna moja isiyo na maana.

11 basi, nisipo ijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.

12 vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.

13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba Lakini akili zangu hazina matunda.

15 Imekuaje basi? Nitaomba kwa roho tena nitaomba kwa akili pia, nitaimba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia.

16 kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje Amina baada ya kushukuru kwako akiwa hayajui usemayo?

17 Maana ni kweli, wewe washukuru uema, bali yale mwingine hajegwi.

18 Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote

19 Lakini katika maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha

20 Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu, Lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima

21 Imeandikwa katika torati, nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni wala hata hivyo hawatanisikia asema Bwana.

22 Basi hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio bali kwao wasioamini Lakini kutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali ni kwa ajili yao waaminio

Neno limesema

“Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana. Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu. Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.

Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

Ukweli ni kwamba, maneno ya lugha, yasipoeleweka, basi hamna mawasiliano. Kusema na lugha isiyoeleweka hutoa maana kwamba mtu asema kwa roho tu Lakini si kwa akili, ajifaidi mwenyewe tu.

Ndiyo sababu Paulo amesema katika mstari wa 18-19
“18. Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote

Lakini katika maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha

Basi hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio bali kwao wasioamini Lakini kutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali ni kwa ajili yao waaminio”

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!