Suluhisho Kwa Lisilowezekana

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Suluhisho Kwa Lisilowezekana
Loading
/
I Wakorintho 15:12-19

Natumai u buheri wa afya, msikilizaji wangu. Jina langu ni David Mungai na ni furaha yangu kukukaribisha tujifunze Neno pamoja, 1 Wakorintho 15:12-19 “SULUHISHO KWA LISILOWEZEKANA”.

Karibu wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena tujifunze Neno pamoja.

Uvumbuzi wa vyombo vya mawasiliano umetuletea mengi yaliyo muhimu na ya maaana sana. Unaweza kuzungumza na mtu akiwa mbali sana, bila shida yo yote. Lakini bado ni tofauti katika akili zetu. Jambo haliwezi kuwa “kweli” na liwe la “uongo” kwa wakati huo huo.

Paulo alikuwa na elimu yake kiasi, na alipojifoa pamoja na elimu yake,kwake Roho Mtakatifu, akaitumia kueneza ukweli wa Injili ya Habari Njema.

Nasoma sasa 1 Wakorintho 15:12-19

12 Basi ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka

14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na Imani yenu ni bure

15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

17 Na kama Kristo hakufufuka, Imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea

19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko wote.

Kunao watu wengine twajua kwamba waliamini kuwa wapendwa wao waliaaga dunia wangefufuka.

Lakini haikuwezekana, Kristo alifufuka siku ya tatu, akaonekana na wanafunzi wake na ndugu zaidi ya mia tano.

Siku ya tatu kaburi lake lilikuwa tupu na nguo zilizomfunga mwili bado zilikuwa kaburini.

Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka, na kuhubiri kwetu, na kuamini kungekuwa bure. Bwana asifiwe Kristo alifufuka.

Kama Kristo hakufufuka ahadi zake kwetu zingekuwa bure.

Mst wa 14 -18

14 Tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na Imani yenu ni bure

15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

17 Na kama Kristo hakufufuka, Imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea

Kwa kifupi Paulo asema kama Kristo hakufufuka basi kuhubiri Injili ingekuwa kazi bure.

Na Imani yetu haingekuwa na maana. Na maisha yetu ya siku za usoni hayangekuwa na tumaini.

Ukweli wa tatu. Kama siyo ufufuo wa Yesu, tungekufa kama farasi au mnyama mwingine. Yaani, tungekufa bila tumaini.

Mstari wa 19

“Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko wote.”

Yaani kama siyo ufufuo wa Bwana wetu Yesu Kristo, hatungekuwa na tumaini la mambo yetu ya wakati ijao.

Tumaini letu hata la uzima wa milele limo, kwa sababu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu, akapaa juu mbinguni na huko ndiko atakapotoka, kuja kulinyakua kanisa la wote wanaomwamini na kukiri kwa mdomo, kwamba yesu ndiye Bwana na mwokozi wetu.

Ni uwongo na ni balaa kwa wasioamini kwamba Yesu Kristo alikufa msalabani na kufufuka siku ya tatu, na baada ya siku arobaini, akapaa mbinguni na katika hali hiyo atatoka huko siku ya kiyama. Kurudi kwake Yesu, Kristo Bwana wetu. Hakuna lisilowezekana kwake Mungu. Mungu alimfufua Yesu Kristo kutoka kwa wafu. Na huu ni ushindi mkuu, kutoka kwake Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!