Msingi Wa Imani Ya Kweli

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Msingi Wa Imani Ya Kweli
/
I Wakorintho 2:1-5

Hujambo na karibu tujifunze Neno pamoja. Leo twalichambua fungu la neno kutoka 1 Wakorintho 2:1-5.
“Msingi wa Imani.”

Jina langu ni David Mungai. Karibu, wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Karibu tena. Hakuna mjengo au nyumba iliyo nzuri kulikom msingi uliyowekwa. Kunao mijengo mingi ambao hubomoka mingine kubomolewa kwa sababu ya kukosa misingi imara. Twaweza kujifunza mengi na mijengo iliyojengwa zamani na mingine ya siku hizi. Kwa mfano majumba ya kihistoria ya misri, pyramid ya Giza. Mjrngo huo ulijengwa miaka zaidi ya 2500 kabla ya kuzaliwa Kristo na hata wa leo huo mjengo umesimama imara. Mjengo huo umejengwa katika ardhi ya ekari 13, na zaidi ya block 2, 300, 0000 na kila block ina uzito wa kilo elfu kumi kila moja. Na kwa sababu ya msingi imara, jumba hilo bado lasimama hata wa leo.

Maisha yetu pia yajitaji msingi imara, katika Mungu. Nasoma Wakorintho 2:1-5 MSINGI WA IMANI YA KWELI.

1 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

2 Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.

3 Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi.

4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
Msingi hujengwa na aina mbalimbali za mawe.

Paulo na Sila walipokuwa gerezani walikuwa wanaimba na kumsifu Mungu. Malaika wa Mungu alishuka akawafungulia kutoka gerezani. Ndipo askari wa jela akawaendea Paulo na Sila na kuwauliza:
Matendo ya Mitume 16:30

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

Wokovu katika Yesu Kristo ndilo jiwe moja linalojenga IMANI YETU KATIKA KRISTO.

Jiwe la pili lapatikana katika Matendo ya Mitume 2:38. “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu

Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Ubatizo kwa roho mtakatifu ni dhihirisho kwamba mtu ameunganishwa na wakristo wengine duniani na ni ishara ya kufa na kufufuka naye Yesu na twangojea kwa hamu kurudi kwake Yesu Kristo. Ubatizo wa Roho na maji ndilo jiwe la pili katika jengo hili – IMANI YETU KATIKA KRISTO.

Jiwe la tatu: NGUVU ZA MUNGU

Katika injili ya Luka 24:49, Kabla ya kupaa kurudi mbinguni aliwaambia wanafunzi wake : “Kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu.”

Na katika Matendo ya Mitume 1:8-9 twasoma: “8. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 9. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.”

Jiwe la tatu. Ni KUTIWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU – KUHUBIRI INJILI KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.

Mfano wa ukweli huo ni Simeoni Petro.

Simeoni Petero na mitume wengine, walikuwa jasiri sana kuhubiri Injili lakini watu wa dini, na serikali ya kivumi walipinga sana uenezaji wa Injili. Lakini kwa ujasiri na nguvu za Roho mtakatifu alisema: Matendo 5:29

29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Ni hakikisho kwamba IMANI YETU KATIKA KRISTO NI DHAKILI NA DHABITI.”

Msingi wa Imani yetu ya kweli umejengwa na mawe matatu.
1.) WOKOVU KATIKA YESU KRISTO.
2.) UBATIZO WA MAJI NA ROHO.
3.) KUTIWA NGUVU NA ROHO MTAKATIFU.