Hudumu Mahali Ulipo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Hudumu Mahali Ulipo
Loading
/
I Wakorintho 7:17-24

Hujambo. Natumai u buheri wa afya, na karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakorintho 7:17-24 – “Hudumu mahali ulipo.” Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam karibu tena. Ni vyema na ni vizuri kuwa katika hali ya kutosheka ni kile Bwana Mungu amekufanikisha kupata. Pamoja na hayo kuwa na akili za kutojali, kufikiria mambo sawa kila mahali na kila saa ni hatari. Ni lazima tuwe na bidi kutumika po pote pale.

Hebu tulitazame fungu hili la Neno, kwa undani tupate kumakinika vilivyo. Wajibika katika shughuli zako. Nasoma Waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho 7:17- 24

17 Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu kama Mungu aklivyomwita kila mtu, na aende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.

18 Je mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu Fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.

19 Kutahiriwa si kitu, na kutotahiriwaq si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.

20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa

21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.

22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.

23 Mlinunuliwa kwa thamani, msiwe watumwa wa wanadamu.

24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbekle za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo.

Hali ni ile ile, yaani fungu hili la Neno, tutafundisha la mke na mume, daima kukaa na kuishi pamoja na kanisa. Matengano hayaruhusiwi.

Na ndivyo anayofundisha hapa. Kama uliokoka na haujatahiriwa tohara si lazima katika wokovu. Iwapo umetahiriwa ni sawa. Ya mwili siyo njia ya kuingia mbinguni. Yesu Kristo ndiye njia na kweli la uzima.

Wito wako katika huiduma kutoka kwa Mungu? Neno lasema hivi. Mstari wa 20-22, 1 Wakor. 7:20-22

20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa

21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.

22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.

Uwe mtumwa mwema kwa waajiri wako kama Danieli na hata Yusufu katika nchi ya Misri. Hata kama boss hayuko, unaye boss anayakutazama kutoka mbinguni. Mpende Kristo zaidi katika shughuli zako, na utazawadiwa vyema kwa uaminifu wako.

Danieli alitumika katika nchi ya kigeni na hata wafalme wa nchi ile, Dario na wenzake wakamheshimu Mungu wa Danieli. Dario akamsaidia Danieli na Wayahudi kujenga ukuta Yerusalemu. Esteri, akiwa mke Mwisraeli aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa mkono wa Namani.

Popote ulipo, dumisha Imani yako. Kwa sababu gani?

Mst. 23-24

23 Mlinunuliwa kwa thamani, msiwe watumwa wa wanadamu.

24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbekle za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. Kwa sababu, tulinunuliwa kwa dhamani. Sisi basi tu mali yake Bwana wetu, Yesu Kristo. Mfalme wa wafalme, alifedheshwa msalabani kwa ajili na kwa sababu ya dhambi zetu, Akalia “Eloi, Eloi lama sabakithani. Mungu Wangu, Mungu Wangu mbona waniacha?” Hayo yote fidia ya moyo wake akalipa upate njia ya Wokovu.

Kweli huyu Yesu, Mfalme Mwokozi na kuhani astahili sifa na kujitolea kwa huduma yake, na kuitekeleza kwa moyo mkunjufu.

Nafikiria wewe msikilizaji kuwa umemwamini Yesu, lakini kama hujafanya hivyo ufanye kama mhabeshi aliyekuwa anatoka Yerusalemu kuabudu lakini bado, hakuelewa Wokovu ni nini, kama tunavyomsoma katika matendo ya Mifune 8:37.

“Filipo akasema: Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.”

Utamtumikia Mungu ukiitikia wito wake, Umtumikie, namna ulivyo maana akuhitaji, katika cheo hicho ulio nacho na po pote ulipo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!