Matumaini Yaliyo Magumu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Matumaini Yaliyo Magumu
/
I Wakorintho 15:35-50

Hujambo na Karibu.

Leo twalichambua neno la Mungu pamoja kutoka 1 wakorintho 15:35-50, namna ya kuelewa na yaliyo magumu.

Jina langu ni David Mungai, wimbo halafu tuendelee.


naam, karibu tena tujifunze neno la Mungu pamoja 1 wakorintho 15:35-50, namna ya kuelewa yaliyo magumu.

Katika Biblia, twajifunza mengi kwa mifano. Na hii ndiyo sababu Yesu Kristo bwan wetu alitumia mifano. Ufalme wa mbinguni ni kama….”

Lakini kwa uwezo na nguvu za Roho Mtakatifu tutalichambua fungu hili la neno 1 Wakorintho 15:35-50,
Nasoma,

35 Lakini labda mtu atasema wafufuliwaye wafu? Nao huja kwa mwili gani?

36 Ewe mpumbavu uipandayo haihuiki isipokufa

37 Nayo uipandayo huupandi mwili ule utakaokuwa ila chembe tupu, ikiwa niya ngano au nyingineyo

38 Lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo na kila mbegu mwili wake

39 Nyama yote si nyama tu, moja, ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege nyingine ya samaki

40 Tena kuna miili ya mbuinguni na miili ya duniani, lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali na fahari yake ile ya duniani ni mbali

41 Kunaa fahari moja ya jua na fahari nyingine ya mwezi na fahari nyingine ya nyote maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota

42 Kadhalika na kiyama na wafu. Hupandwa katika uharibifu hufufuliwa katika kutoharibika

43 hupandwa katika aibu hufufuliwa katika fahari hupandwa katika udhaifu hufufuliawa katika nguvu.

44 Hupandwa mwili wa asili hufufuliwa mwili war oho. Ikiwa uko mwili wa asili na war oho pia uko.

45 Ndivyo ilivyoandikwa, mtu wa kwanza adamu akawa nafsi iliyo hai Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha

46 Lakini hautangulii ule wa roho bali ule wa asili baadaye huja ule war oho

47 Mtu wa kwanza atoak katika nchi, ni wa udongo, mtu wa pili atoka mbinguni

48 Kama alivyo yeye wa walio wa udongo na kama alivyo yeye wa mbinguni ndivyo walivyo, walio wa Mungu

49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni

50 Ndungu zangu, nisemayo ni haya ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu wala uharibifu kurithi kutokuharibika

Katika Mungu hili la neno la mungu, Paulo atueleza yaliyo muhimu lakini hatuwezi kuyaelewa kwa akili zetu. Twaweza tu kujitwalia kwa Imani, kwamba katika Kristo Yesu mna ufufuo.

Na hii ndiyo sababu Yesu Kristo, akiwa Mungu alichagua kuyakamilisha watakuwa ya Mungu baba ya utaratibu na mpango wa wokovu huu ulivyo mkuu

Ukuu wa wokovu na kama alivyo Mungu. Ni mapenzi yake Mungu sisi kama wanadamu tujitwalie wokovu kuokolewa kutoka dhambini hatuwezi kujiokoa. Kutoka dhambini na Mungu akaona hivyo.

Wokovu wetu umebeba mambo mengi makuu ingawa bado tu wanadamu nab ado tuko ulimwenguni huu wa dhambi kwa Imani twawezaa kujitwalia nguvu za ushindi kwa kumwapisha Roho mtakatifu mioyoni mwetu.

Mkristo kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu na watu wake wakawekwa Safina wakaokolewa na gharika ndivyo tumeokolewa na kifo cha kiroho. Kifo cha mwili ndio lakini roho zetu hatima yake ni mbinguni.

Anayemwamini Yesu hataingia katika dhiki kuu ya miaka saba baada ya kunyakuliwa kwa kanisa lake

Wokovu wetu katika Yesu hutupatia nguvu za kuitwa watotot wa Mungu na baada ya dhiki kuu tutarudi na

Kristo duniani ili atushirikishe katika ufalme wake wa miaka elfu. Hatimaye itakuwa furaha tele pamoja na Yesu milele na milele.

Twajitwalia hayo yote kwa kutubu dhambi zetu kwake Yesu na kumpokea moyoni. Siku ya kuokolewa ni sasa.