Meza Ya Bwana

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Meza Ya Bwana
Loading
/
I Wakorintho 10:16-22

Msikilizaji mpendwa, nakusalimu katika jina la Yesu hujambo? Karibu tujifunze Neno la Mungu pamoja kutoka 1 Wakor 10:16-22 – “Meza ya Bwana.” Jina langu ni David Mungai. Wimbo, halafu tuendelee.

Naam, Karibu tena. Twalichambua fungu la Neno la Mungu kutoka 1 Wakorintho 10:16-22.

Tunaposhiriki katika Meza ya Bwana, sharti lazima tukumbuke ya kwamba si jambo la majuzi, lakini lilianzishwa na Mungu mwenyewe likaitwa Pasaka katika kitabu cha Kutoka 12:1-14. Waisraeli walikumbuka kukombolewa kwao kutoka nchi ya Misri.

Kila mtu alimtwaa mwanakondoo, ambaye hana ila, mume wa mwaka mmoja.

Waliikula, nyama yote ya yule mwana kondoo, na mboga zenye uchungu siku ya kumi nan ne ya mwezi wa kwanza. Walikula na mikate isiyotiwa chachu. Walikula nyama choma wasiibakishe kitu.

Waliikula ile nyama, wamefungwa viuno, viatu miguuni, fimbo mikononi, walikula kwa haraka, ni Pasaka ya Bwana. Alipozaliwa Yesu, aliendeleza ufunuo, akazaliwa na bikira, akauchukua mwili wa kibinadamu, akaishi kwa ukamilifu na akajitoa kwa sababu ya kutupenda akawa kondoo wa Mungu dhabihu kamilifu kwa ajili ya dhambi zetu. Kama alivyouawa mwana kondoo; Kristo akafa akamwagwa damu tupate ondoleo la dhambi.

Nasoma sasa 1 Wakorintho 10:16-22

16 Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao si ushirika wa mwili wa Kristo?

17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya yule mkate mmoja.

18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili, wale wazilao dhabihu je! Hawana shirika na madhabahu?

19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?

20 Sivyo, lakini vitu vyote vile wavitoavyo sadaka, wavitoa kwa mashetani wala si kwa Mungu, name sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22 Au twamtia Bwana wivu? Je, tuna nguvu zaidi ya yeye?

Mtume Paulo, hapa atuonyesha ya kwamba meza ya Bwana ni yake, Bwana. Na ni ya kila anayemwamini Yesu apate kushiriki. Meza ni chakula cha Bwana Yesu. Ni wakati wa kushirikiana, moja na mwingine, wote wamwabudu Mungu. Na huu ni ukweli wa Meza ya Bwana, hiki ndicho chakula Bwana, cha ukumbusho.

Mst 16-17. “Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

Meza ya Bwana ni ushirika wa wakristo wote. Na kama ilivyokuwa kweli katika Agano la kale ndivyo ilivyo katika Agano jipya.

Kwa hiyo, hatupaswi kusherehekea meza ya Bwana kama wasiyomjua Mungu bali kama tunayemwabudu Mungu wa kweli, tusiabudu kama wasiyomjua Mungu. Tusishirikiane na ibada za shetani, hamwezi kunywea kikombe cha mashetani.

Tunaposhiriki katika meza ya Bwana, twamkumbuka Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyoutoa uhai wake msalabani ili tukitubu na kumwamini, twamwabudu, twampa nafasi ya kwanza maishani mwetu.

Meza ya Bwana ni ushirika wa mwili wa Kristo. Kanisa lake duniani kote kwa wote wanaomwamini na kumpokea, haijalishi dhehebu wa taifa? Kama ilivyo kwamba Kristo aja, arudi kulinyakua kanisa lake.

Tujitayarishe kwa kumpokea Bwana arudipo kutunyakua kwa kumwamini na kushirikiana katika mwili wake. Kanisa la waumini wote. Meza au ushirika ni wa kila anayemwamini Yesu Kristo, tuache ubaguzi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!