Huduma Za Mwili

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Huduma Za Mwili
Loading
/
I Wakorintho 12:27-31

Hujambo na Karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakorintho 12:27-31
“HUDUMA ZA MWILI” Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee

Naam, Karibu tena, twalichambua fungu la 1 Wakorintho 12: 27-31, huduma ya mwili wa Kristo

Kanisa ndilo mwili wa Kristo, na kila kiungo ni cha maana na sisi ndio viungo vya mwili huo. Ni muhimu kujitwalia ukweli huu. Kila mkristo na ajue na kuamini ukweli huu. Kila mkristo na jue na kuamini ukweli huu. Nasoma sasa,

27 Basi m=ninyi mmekuwa mwili wa Kristo na viungo kila kimoja peke yake

28 Na Mungu ameweka wengine katika kanisa wa kwanza mitume wa pili manabii wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano na maongozi , na aina za lugha

29 Je, wote, ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu wote wanatenda miujiza?

30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wasafiri?

31 takeni sasa karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora

Katika fungu hili la neno twapata huduma mbalimbali na wahudumu mbalimbali

Twapata mitume, neno hili lilitumiwa kwanza kwa mitume ya Bwana wetu Yesu Kristo, mitume waliotumwa kuwapeleka watu wengine ujumbe.

Mitume wa kwanza twawasoma, katika injil ya Mathayo 10:2-4

Na majina wa hao mitume kumi na wawili ni haya wa kwanza ni simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye, Yakobo wa Zebedayo na Yohana nduguye

Filipo, na Bartholomayo, Tomaso wa Alfayo, na Thadayo, 4 Simoni Mkananayo na Yuda Iskarioti na ndiye mwenye kumsaliti

Mstari wa 5 waonyesha maana na sababu, wanaume wale kuitwa mitume hao thenashara, Yesu aliwatuma akawaagiza, akisema. Katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wote wote wa wasamaria msiingie mst 7…”na katika kuenenda kwenu, hubirini mkisema ufalme wa mbinguni umekaribia

Mtume, hutumwa na mwenyezi Mungu kueneza ujumbe wa ufalme wa Mungu. Mtume wa kujituma si mtume. Mitume kama hao wametajwa katika 2 Wakorintho 11:13

Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo

Pili, tunaomanabii. Hata waleo, twawatambua manabii waliotajwa katika agano la Klae. Eliya, Yeremia, Isaya, Yona, Samueli, na Danieli.

Hata nabii Isaya na Eliya wametajwa katika Agano Jipya. Nabii katika agano la kale, aliyatabiri ya siku zijazo na hapo lazima tuelewe ya kwamba nabii sharti ayatabiri yanayoambatana na neno la mungu si kinyume. Neno hili nabii limetajwa mara 161 katika agano jipya

3 tunao waalimu mwalimu wa neno la Mungu na kutenda siyo kuhubiri au kufundisha kwa maneno tu. Fundisha neno kwa maneno na matendo nikodemo aliutafuta ukweli, wa namna mtu anaweza kuzaliwa upya

Wengine ambao wametajwa ni, watenda mijiza karama za kuponya maisindiano maongozi na aina za lugha. Na tunapovitumikishe kwa umoja wa mwili wote wa kanisa la Bwana Yesu Kristo.

Hata hivyo mst 31 takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. Na njia hiyo yaonyeshwa katika 1 Wakorintho 13, sura ya upendo. Yaani tuvitumikishe talanta na vipawa vyetu kwa upendo. Tusichoke kutenda mema, na kwa upendo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!