Kukudumu Pamoja

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kukudumu Pamoja
/
I Wakorintho 16:13-24

Msikilizaji wangu mpenzi natumai u buheri wa afya na karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakor 16:13-24, “TUKUDUMU PAMOJA”. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena tujifunze Neno. Twalichambua fungu la Neno 1 Wakor. 16:13-24. “TUKUDUMU PAMOJA”

Historia ya kanisa yaonyesha wanafunzi wake Yesu, hata wale walikuwa vigumu kuamini Yesu alifufuka, hatimaye waliamini na kuitikia wito wa kueneza injili. Tomaso akaenda India hata kuna kanisa nchini India kwa jina-Mtakatifu Tomaso. Yohana, aliyeitwa Mariko akaenda Misri safari ya kuhubiri habari njema ya wokovu katika Kristo Yesu. Na kanisa likaenea katika utawala wa kirumi. Hata karibu na bahari, na bahari ya chumvi, kaskazini, magharibi, kukawa na kikundi cha watu waliojitenga kuwa watakatifu.

Kundi hilo Qumran, lilijitenga na watu wengine wakitetea utakatifu wao. Wafarisayo nao waliwaiga kunid lile kwa kuweka Torati na sharia. Lakini Yesu akawaambia: Mathayo 15:17-20.

17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni, navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wivu, ushuhuda wa uongo na matukano,

20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi, lakini kula kabla hujanawa mikono hakumtii mtu unajisi.

Maneno hayo yaonyesha wazi, kwamba kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kujiweka watakatifu. Jibu twalipata katika waraka wa Paulo kwa Warumi 12:1-2

1 Basi ndugu zangu nawasihi, kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.

Nia zetu hufanywa upya kwa kujitwalia, ukweli wa Neno la Mungu. Nakuomba uwe na uzoefu wa kulisoma Neno la Mungu, Biblia ulitafakari na kujitwalia ukweli wa hilo Neno. Neno la Mungu ndilo dawa ya kutakasa nia zetu.

Nasoma sasa Neno kutoka 1 Wakor 16:13-24

13 Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.

14 Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

15 Tena ndugu nawasihi, mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefano, kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu,

16 watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kustaajabisha.

17 Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefano, na Fortunato na Akaiko, maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu.

18 Maana wameniburudisha roho yangu na roho zenu pia, basi wajuane sana watu kama hao.

19 Makanisa ya Asia wanawasalimu. Akila na Priska wanawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.

20 Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

21 Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe.

22 Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha (Bwana wetu anakuja).

23 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi

24 Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.
Ili tuhudumu pamoja lazima na ni muhimu kuudumisha upendo. Katika vita vya kiroho, Paulo atuamuru,

“…kesheni, simameni imara katika imani fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.”

Tuwe macho tukisimama katika misingi, Neno la Mungu! Wacha kuutegemea uvumi, wa watu. Tafuta na ukalie ukweli wa Neno la Mungu.

Bega kwa bega, tuhudumu pamoja, kwa unyenyekevu ndugu na mwingine, kwa kuchukuliana mmoja na mwingine, pamoja tutapata ushindi.

Pamoja na hayo, tupalilie undugu wetu kwa kujuliana hali. Waamkue watu wa Sharika, mpate kushikiana kwa upendo. Ukiweza, kama imeruhusiwa na mila na desturi, unaweza kumbusu au kumkumbatia ndugu au dada katika busu takatifu. Maranatha. Kristo yuaja upesi. Basi Paulo atoa onyo.

Katika mstari wa 22, twapata Neno hili:

‘Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa-naja upesi.’

Kwa kifupi au kirefu, haijalishi asiyemwamini Yesu, amehukumiwa kutupwa kuzimu, na hatimaye katika bahari ya moto uwakao na kiberiti.

Mwamini Yesu upate kunyakuliwa pamoja na Wakristo wengine Kristo arudipo kulinyakua kanisa lake. Kristo arudi kutuchukua ili alipo nasi tuwepo.