Ushauri Kwa Sharika Zetu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ushauri Kwa Sharika Zetu
Loading
/
I Wakorintho 16:1-12

Hujambo msikilizaji mpenzi, na natumai u buheri wa afya. Shukran kwa mwenyezi Mungu. Karibu tujifunze neno pamoja. 1 Wakorintho 16:1-12 ushauri kwa sharika zetu. Jina langu ni David Mungai wimbo halafu tuendelee.

Naam, karibu tena twalichambua, fungu la neno kutoka 1 wakorintho 16: 1-12 ushauri kwa sharika zetu.

Mtume Paulo aliwafundisha wakorintho yale yote aliwafundika washiriki wa aliwafundika washiriki wa makanisa au shaika zote alizoanzisha bila unbaguzi n ahata waleo mafundisho ya waraka huu kwa wakorintho ni muhimu kwa kila sharika hata wa leo. Hebu sikiza vile alivyoliambiua kanisa la kivumi sura 14:12

Basi ni hivyo kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Sasa nasoma kutoka 1 Wakorintho 16:1-12

1 Kwa habari ya ile chagizo kwa ajili ya watakatifu kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo

2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na kadiri ya kufanikiwa kwake ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja

3 Nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua wachukue hisani yenu mpaka yerusalemu

4 Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami

5 lakini nitakuja kwenu nikiisha kupita kati ya makedonia maana napita kati ya makedonia

6 labda nitakaa kwenu naam labda wakati wote wa baridi mpate kunisafirisha kokote nitakapoenda

7 maana sipendi kuonana nanyi sasa katika kupita tu kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo bwana akinijalia

8 lakini nitakaa Efeso hata pentekoste

9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana na wako wenfi wanipingao.

10 lakini timotheo akija angalieni akae kwenu pasipo hofu maana anaifanya kazi ya bwana vile vile kama mimi mwenyewe

11 basi mtu ye yote asimmdharau lakini msafirike kwa Amani ili aje kwangu maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu

12 lakini kwa habari za Apollo ndugu yetu nalimsihi sana aende kwenu pamoja na ndugu amabaye si mapenzi yake kwenda sasa lakini atakuja atakapopata nafasi

Fungu hili la neno lafundisha mambo muhimu tunayopaswa kufanya katika sharika zetu

Mst 1-4 ni muhimu kuchukua sadaka ili tuweze kuwasaidia ndugu . na hivyo ndivyo alivyolifunza na kanisa la Galatia mst 1

Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu kama vile nilvyoamuru makanisa ya Galatia ninyi fanyeni hivyo

Jambo la pili uwakili mwema mst 2 siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake kwa kadiri ya kufanikiwa kwake ile kwamba michango ifanyike hapo nitakapokuja tutoe kwa akili kulingana na kug=fanikiwa kwetu tuwajali na wengine katika kanisa

Jambo la tatu. Tutoe kulingana na mapato yetu. Kwa kweli mungu anastahili shukrani za sadaka maana upendo wake haupimiki tutoe kwa mioyo mikunjufu

Tumejifunza ya kwamba ni muhimu kutoa sadaka tuweze kuwasaidia ambao hawawezi kati yetu

2 tuwe mawakili au mabalozi waaminifu

3 na tuwe wakarimu katika kutwa kwetu bila kusukumiwa maana upendo wake haupikimiki na hauna kifani. Uwe na mpangalio mzuri wa safari zako za injili

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!