Huduma Ya Roho

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Huduma Ya Roho
Loading
/
I Wakorintho 12:1-11

Hujambo, msikilizaji na karibu tujifunze Neno. Leo twalichua fungu la Neno kutoka 1 Wakor. 12:1-11. “HUDUMA YA ROHO.”

Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee kujifunza.

Karibu tena tujifunze Neno kutoka 1 Wakor. 12:1-11 : “ Huduma ya Roho”. Mengi yamesemwa na kufundishwa kuhusu huduma hii ya Roho; na katika kipindi tutajaribu kuelewa Neno lasemaje na hata kufundisha. Nasoma: 1 Wakor. 12:1-11.

1 Basi ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.

2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.

3 Kwa hiyo nawaarifu ya kwamba, hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema Yesu amelaaniwa, wala haezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, asipokuwa katika Roho mtakatifu.

4 Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule.

5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana

8 Maana mtu mmoja kwa roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule.

9 Mwingine Imani katika Roho yeye yule, na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja

10 na mwingine matendo ya miujiza, na mwingine unabii, na mwingine, kupambanua roho; mwingine aina za lugh; na mwingine tafsiri za lugha,

11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.”

Kwanza kabisa, ningependa tuelewe ya kwamba, Karama za kiroho, ni uwezo ambao Mungu huwapa wanaomwamini Yesu Kristo, yaani Wakristo, ili wamtumikie. Kila Mkristo anao karama, kama tunavyosoma katika 1 Petro 4:10

“Kila mmoja kwa kadiri alivyopokea karama, itumieni kwa kuhudhumiana; kama mawakili wema wa neema mbali mbali za Mungu.”

Katika kanisa la Korintho, karama zote zilikuwepo kati ya waamini wote.

Katika sura hii ya 1 Wakor. 12 mpaka 14, Paulo afundisha kuhusu karama hizi, za kiroho, maana katika lile kanisa kulikuwa na mgawanyiko.

Na 1 Wakor. 13, ni sura ile tunayoijua sana ya upendo. Yaani karama zote katika huduma ya Mungu., zitumikishwe kwa upendo, na katika sura ya 14, ywapata karama maalum unabii na kusema kwa lugha.

Katika aya ya 8-10, twapata maneno mawili, yanayohitaji ufafanuzi zaidi Neno “hekima” na “maarifa”.

Neno “hekima” yamaanisha mwasiliano katika hekima ya kiroho, na hii hutokana na Mungu mwenyewe, anapowasiliana nasi katika na kwa neno lake.

Neno “maarifa” ni mawasiliano ya ukweli unaotenda kazi. Ukweli unaotendeka katika vitendo vyenye hayo maarifa ya Neno la Mungu, huzaa Imani. Imani katika Neno la Mungu, yaani unaposoma Neno, wewe waamini ya kwamba Mungu ni mwaminifu katika kumakinisha linavyosema Neno.

Yaani kutoka kwa ujuzi wako wa neno, wamtegemea na anavyosema katika Neno lake.

Pamoja na hayo twapata karama za uponyaji, kuhuishwa, na unabii, jinsi tunavyotangaza funuo kutoka kwake Mungu, lazima zikubaliane na anavyosema Mungu katika Neno lake, na ule ufunuo utekelezwe kwa upendo.

Na katika mstari wa 10, twapata, karama ya kusema na lugha mpya na uwezo wa kutafsiri utafsiri ni muhimu, ili na Wakristo wengine katika sharika waupate ujumbe mpya, ili kanisa lipate kukua pamoja, la sivyo, lugha hizo zitamkuza mtu mwenyewe binafsi. Hata hivyo, lazima tuelewe ya kwamba, hizi lugha zilikuwa muhimu sana kabla ya kuweko Neno la Mungu Bibilia.

Karama hizi zote ni muhimu sana katika uhusiano wetu mmoja na mwingine katika kundi la waumini. Maana tu viungo vya mwili wa Kristo, ambao ni kanisa la kiroho. Kila mmoja wetu amhitaji mwenzake, na kama vile tumeonyeshwa katika sura ya 13- Lazima tukae, tuishi, na tuhudumiane kwa upendo. Upendo ambao, hauhusudu, hauna chuki, iliwe hesabu mabaya, na kadhalika. Twahitaji kuchukuliana katika mambo yote, na huduma ya Injili itaimarika kati yetu na kueneza duniani kote.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!