Unabii Kipau Mbele

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Unabii Kipau Mbele
Loading
/
I Wakorintho 14:1-9

Msikilizaji natumai u buheri wa afya na karibu tujifunze Neno la Mungu pamoja. 1 Wakorintho 14:1-9.
“UNABII UPEWE KIPAU MBELE” Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena. Leo twalichambua Neno kutoka 1 Wakorintho 14:1-9. Unabii upewe nafasi ya kwanza.

Kanisa la Korintho, lilianza kwa shida, maana wayahudi walipinga sana uenezaji wa Injili ya Bwana Yesu, kwa sababu haikuhimiza utendaji wa sheria. Wakristo wakapelekwa mahakamani, lakini hakimu, Gallio akatupilia mbali kesi kwa sababu mashtaka yalikosa msingi. Habari hizi twazipata katika matendo ya mitume 18:14-15.

Nasoma matendo ya mitume 18:14-15

14 Na Paulo alipopata kufunua kinywa chake, Galio akawaambia wayahudi kama lingekuwa jambo la dhuluma au la hila mbaya, enyi wayahudi, ingekuwa haki mimi kuchukuliana nanyi,

15 bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sharia yenu liangalieni ninyi wenyewe maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo.”

Sasa basi, tulitazame Mungu kutoka 1 Wakorintho 14:1-9

1 Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu,

2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu, maana hakuna asikiaye lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

3 Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji na kuwatia moyo.

4 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye nilijenga kanisa.

5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

6 Ila sasa, ndugu nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo au kwa njia ya hotuba au kwa njia ya fundisho?

7 Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni filimbi, ikiwa ni kinubi, visivyotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani uliopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

8 Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, ni nani atakayejifanya tayari kwa vita?

9 Vivyo hivyo, na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.”

Tuufuate upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba tupate kuhutubu. Tuhutubu ya Mungu na Neno lake.

Maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu, bali husema na Mungu, maana hakuna asikiaye, lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga na kuwafariji, na kuwajia moyo.

Hotuba za kufariji afadhali. Na ni nyingi katika Biblia. Kwa mfano: katika kitabu cha mwanzo 17:19.

Mungu alimwahidi Ibrahimu, na mkewe Sarai ingawa walikuwa wamepita umri wa kupata watoto, Mungu aliwapa hotuba ya habari njema. Ujumbe wa kuwafariji.

“Mungu akasema, sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume nawe utamwita jina lake, Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake badala yake.”

Na twaona ya kuwa agano hilo, Mungu alilifanya imara na kulikamilisha katika kitabu cha mwanzo 21:1-2.

Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na, BWANA akamfanyia kama alivyosema.

Mst. 2 “Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

Hotuba za unabii kama hii, italifaidi kanisa na kuimarisha imani ya wengi kiroho. Eliya pia alitoa hotuba ya kunyesha kwa mvua, na ikawa hivyo. Ahabu akasafiri mbio, asinyeshewe na mvua.

Hayo yatuonyesha ya kuwa twaweza kutilia maanani hotuba za unabii, na hotuba hizo, ziwe zimekubaliana na mapenzi ya Mungu. Unabii wa kweli hukuza kanisa, nah ii ndiyo sababu Paulo asema hivi katika maneno ya 4-6. 1 Wakor 14:4-6

4 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye hulijenga kanisa.

5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha lakini zaidi sana mpate ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

6 Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya elimu au kwa njia ya hotuba au kwa njia ya fundisho?

Basi tuyazingatie ya Neno, hotuba zinazojenga.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!