Ukoo Wa Daudi

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ukoo Wa Daudi
/
Warumi 1:1-7

Hujambo na karibu, Jina langu ni David Mungai, msalimu wako wa neno. Leo twaliangalia kwa undani ukoo wa daudi kama tunavyosoma kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 1:1-7. Wimbo, alafu tutaendelea

Wimbo

Karibu tena. Warumi 1:1-7. Ukristo ni tofauti sana na dini zingine. Imani yetu I wazi siyo wazo au mawazo ya binadamu. Katikati mwa imani yetu, tunaye mwana wa mungu, yesu Kristo wa nazareti na huyo ndiye ujumbe tunaokuletea wewe msikilizaji mpenzi. Kristo Bwana ndiye msingi wa imani yetu.

Nasoma fungu hili la neno la mungu, warumi 1:1-7

1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;

2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu;

3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,

4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;

5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;

6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo;

7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.

Ukoo wa daudi,

Kutoka kwa ukoo wa daudi, manabii walimtabiti yesu. Nasoma mwanzo 12:3

Name nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani na katika wewe jamaa zote wa dunia watabarikiwa.

Na katika kumbukumbu la torati, 18:15, musa alisema, Mungu atamtoa nabii kama yeye. Na katika 2 samueli 7:16 nabii nathani alimwambia Daudi ya kwamba mungu atamteua mtu kuketi katika kiti chake cha enzi, Jambo la kupendeza kweli.

Katika zaburi 89:35-37, Daudi amshukuru Mungu kwa sababu atamwapisha kuwa mfalme atakayetoka kutoka kwa ukoo wake.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika chuo cha nabii yeremia 23:5-6 na 33:55 na hata katika chuo cha nabii isaya 11:10. Isaya atabiri vivyo hivyo. Kutoka kwa ukoo wa Daudi, masihi atatokea na huo ndio ukweli, kwamba masis Yesu Kristo alitokea ukoo wa Daudi.

Na katika warumi 1:3 neno latangaza kwa uweza na mdiye msingi wa wokovu

3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,

4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;

Mahali kwingi katika neno lake Mungu, uweza wake masihi, yesu kristo umedhihirishwa na kwamba atazaliwa na bikira Mariamu, kufuatana na kulingana na roho wa utakatifu, maana yake utakatifu, maana yake ni kwamba Yesu alizaliwa wala hakutenda dhambi

Hata hivyo aliangikwa kwaajili na kwa niaba yetu sis weny e dhambi ili kwa kifo chake tupate onfoleo la dhambi atakufanya mwenye haki na kujitwalia amani ya moyoni. Na hiyo amani hudumu mioyoni mwetu kwa njia ya kumwamini yesu kristo. Tumshukuru na kumtukuza maana ndiye mfalme wa amani na kwa kumwamini huyo Yesu, sisi hujitwalia amani hiyo maana twasadiki kwamba mfalme wa amani yu nfani na kati yetu.

Yesu aliye wa ukoo wa Daudi yunasi nay u ndani yetu. Mwamini Yesu kristo masihi aliye Mfalme wa amani na ndiye Bwana na mwokozi wa kila anayemwamini.