Mawazo Yake Paulo Kuhusu Israeli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mawazo Yake Paulo Kuhusu Israeli
Loading
/
Warumi 9:1-5

Hujambo na karibu. Leo twalitazama neno la Mungu makini kabisa , Waraka wa Paulo 9:1-5. ‘MAWAZO YAKE PAULO KWA WAISRAELI’ Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Twachambua fungu la neno la Mungu kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 9: 1-5

Kila mmoja wetu anazo fikra mawazo hata hisia. Twawafikiri watu wa familia tunaofanya kazi nao nasi huwasiliana kwa njia nyingi tofauti. Na hivyo ilivyokuwa na Paulo alipowaandikia Wakristo Warumi waraka huu. Hangeweza kuachilia hisia zake bila kuwawaza Waisraeli. Na kutoka kwa fungu hili twayapata mawazo yake Paulo kuhusu Waisraeli.

Paulo mwenyewe alikuwa Mwisraeli na alilijua na kulifahamu neno hasa kutoka ngano la kale. Alikuwa na bidi sana kuwaletea, Waisraeli habari njema. Mawazo na nia nzuri. Nasoma sasa Waraka wa Paulo kwa Warumi, 9:1-5

1 Nasema ukweli tupu; nimeungana na Kristo nami sisemi uongo. Dhamiri yangu ikiongozwa na Roho Mtakatifu inanithibitishia jambo hili pia.

2 Nataka kusema hivi: Nina huzuni kubwa na maumivu yasiyopimika moyoni mwangu

3 kwa ajili ya ndugu zangu walio wa taifa langu! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.

4 Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; alifanya nao maagano, akawapa sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.

5 Wao ni wajukuu wa mababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamu wake, ametoka katika ukoo wao. Mungu atawalaye juu ya yote, na atukuzwe milele! Amina.

Kwanza kabisa Paulo atamwambia vile atakavyotamani. Mstari wa tatu “Kwa maana mngeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa kwa ajili ya ndugu zangu; jamaa zangu kwa jinsi ya mwili.”

Naweza kumfananisha na Musa. Waisraeli walipomwasi Mungu kwa kujitengenea sanamu. Mungu alikasirika sana; pale mlimani Sinai. Mungu alitaka kuwaondoa Waisraeli wote. Musa alimwendea Mungu na kumwambia. Kitabu cha kutoka 32:32

“Walakini sasa ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute nakusihi katika kitabu chako ulichoandika.

Hari ya Paulo ilikuwa kama ya Musa. Alijitoa kuwalinda na kuwatunza watu wa taifa lake hata mbele za Mwenyezi Mungu. Na Paulo hukuacha kuwadhamini watu wake Israeli. Alitamani san ahata baada yake kukutana na Bwana Yesu njiani akienda Dameski kuwatesa waliomwamini Yesu Kristo. Hebu tuangalie maneno ya mstari wa 4 na wa tano.

“Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; alifanya nao maagano, akawapa sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake. 5Wao ni wajukuu wa mababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamu wake, ametoka katika ukoo wao. Mungu atawalaye juu ya yote, na atukuzwe milele! Amina.”

Ni kama ile utukufu aliowaonyesha jangwani. Mungu akawachukua Waisraeli, atawafanya wanawawe akawawekea utukufu uluonekana katika Sanduku la Bwana Mungu, jangwani. Akafanya agano na Waisraeli, akawapa torati, iliyoonyesha utakatifu wa Mungu , na hata huduma yake Mungu. Mungu akawafanya Waisraeli mawakili wake duniani. Pamoja na hayo, Bwana Yesu alizaliwa katika nchi ya Uyahudi –Israeli. Walimiminiwa Baraka nyingi. Hizo Baraka ni zetu pia tukiwa ndani ya Yesu maana aliyakamilisha yote ya torali kwa ajili yetu. Si ajabu Paulo aliyawaza makuu kuwahusu Wayahudi, kwa sababu walipaswa kumwakilisha Mungu duniani lakini yakawa kinyume. Yesu akajitoa kufa ailipe gharama ya dhambi zetu tukitubu tupate ondoleo la dhambi tuwe waridhi wa Mbinguni

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!