Nikiwa Na Mungu Niko Sawa

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Nikiwa Na Mungu Niko Sawa
/
Warumi 8:31-39

Hujambo na karibu. Jina langu ni David mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi cha matumaini, leo twalichambua neno la mungu kutoka Warumi 8:31-39, nikiwa na mungu niko sawa. Karibu wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena leo twalichambua neno la mungu kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 8:31-39 nikiwa na mungu niko sawa

Siku moja kulikuwa na mkutano wa injili na kulikuwa na dada mmoja aliyependa sana kuhudhuria ule mkutano wa injili. Lakini makusudi mwajiri wake alimpa kazi nyingi ofisini dada mcha mungu alijaribu kumaliza ile kazi mapema lakini akashindwa hata hivyo alipomaliza mkutano ulikuwa umekwisha

Kabla ya safari kwenda nyumbani alimwomba mungu amlinde katika safari. Ni usiku giza limeingia kabla ya kufika kwake nyumbani ilibidi apitie msituni ilikuwa hatari wakora na wanyanganyi walikuwa pale walikaa pande za barabara. Dada akatembea njiani wakora walifuata tu kam kusindikiza wakaupata ule msitu hakuana aliyethubutu kumptupia yule dad ahata jiwe. Kila wakijaribu kumdhuru dada wailishindwa. Akafika kwake nyumbani wakora wakamfwata yule dada wakambishia mlango, mlango ukafunguliwa. Wakamuuliza yule dada kwani yeye ni mtu wa aina gani, tumejaribu kukushambulia pale msituni tukashindwa

Daada akwaambia ah, mimi sina habari wala sikujua kuna mtu alinifuata. Lakini kama mwasema ukweli basi ni bwana yesu aliyenikinga na ulinzi wake, akawapa wale majambazi chai wakaenda zao

Mkristo uko sawa mikononi mwa yesu bwana wetu. Nasoma sasa kutoka warumi 8:31-39

31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.

35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.

37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Yesu akiwa nasi hakuna wakutupinga na akiwepo wa kutupinga vita si vyetu ni vya bwanayesu mwokozi na mlinzi wetu. Yesu akiwa pamoja nasi, hakuna wa kutushtaki

33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

Ni shetani ndiye hutushtaki Mbele ya mungu lakini ameshindwa na damu ya yesu. Shetani hana chake bwana asifiwe sana na hakuna anayeweza kutuondoa katika upendo wa mungu hata kifo na maadui wengine hawawezi

Hamna wakushtaki tuna ulinzi tosha katika yesu leo n ahata mileletuko salama mikononi mwake