Sababu Ya Kukosa Imani

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Sababu Ya Kukosa Imani
Loading
/
Warumi 1:24-32

Hujambo na karibu. Leo twalichambua neno kutoka kwa waraka na Paulo kwa Warumi 1:24-32. “SABABU YA KUKOSA IMANI.”Jina langu ni David Mungai. Furahia huu halafu tuendelee.

(WIMBO)

Naam. Karibu tena. Twaweza kulinganisha maisha na njia au barabara,na nyakati zingine sisi hupotea hatujui tuendapo barabara zingine huwa na mabonde,milima mashimo na kadhalika.

Hata hivyo kunazo vibao vinavyo msaidia mtu,uja alipo na aendako. Lakini nyakati zingine hatujui tuendako maana tumekosa Imani ya tuendako na tumepotea njia.

Imani yetu haipo,na tukikosa imani hatufui dafu katika safari. Katika Warumi 1:24-32,Paulo asema.

24 Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao.

25 Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina.

26 Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile.

27 Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu.

28 Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.

29 Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya,

30 na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii wazazi wao;

31 hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine.

32 Wanajua kwamba Sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.

Sababu ya kukosa Imani au kua na upungufu wa Imani zimeonyeshwa wazi katika kifungu hiki cha neno.

Mtu anakuwa mwenye Imani haba,anapoanza kuabudu tamaa zake za mwili wako.

Neno limesema.

24 mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao,waufuate uchawe hata wakavunjiana heshima miilini.

23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu wa ndege na wanyama na vitambaavyo.

Mtu anapokua na Imani haba ni rahisi sana kuruhusu vitu na tamaa kuchukua mahala pa Mungu moyoni.

2 imani yetu inapopungua Mungu hutuachilia kufuata tamaa zetu za aibu,hata wanawake kubadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili ya wanaume vivyo hivyo.

Mambo hayo yatendeka kati yetu kwa sababu ya kukosa kushikilia Imani vilivyo. Ndiposa twayasoma na kuyasikia mengi kuhusu usoga

Imani yetu ni haba,tunapoangukia na kujiingiza katika mambo hayo. Ni chukizo na dhambi tunapojiingiza katika mambo hayo. Dawa ni kutubu na kuungama dhambi hiyo.

3 imani hafifuu hutufanya wakaidi kama tunavyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,wayafanye yaliyowapasa.

Na hii ndio sababu jamii na familia,shirika zetu zimejaa Udhalimu wa kila namna

Uovu na tamaa na ubaya

Tukiyazingatia yaiyo katika neno la Mungu kwa mioyo ya dhati basi tutaijenga imani yetuna kumkinika katika kuishi maisha yanyomcha Mungu na kwa utakatifu wake “mungu tukingojea kwa hamu siku ya kiama”

Basi tujifunze kumwabudu kwa mioyo mikunjufu tumpe Mungu nafasi ya kwanza mioyoni na maishani mwetu.

Naomba Mungu atupe njaa na kiu la neno lake,tumjue na kuamua kumwapisha Mungu maishani mwetu. Na kumpa nafsi ya kwanza

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!