Ujumbe Wa Gabrieli – Neno La Kweli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ujumbe Wa Gabrieli – Neno La Kweli
Loading
/
Danieli 10:10-21

Salaam. Msikilizaji wangu mpendwa. Karibu tujifunze Neno pamoja. Chuo cha Nabii Danieli 10:10-21.

UJUMBE WA GABRIELI – NENO LA KWELI

Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo, alafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena tujifunze Neno. Danieli 10:10-21. Ninasoma:

10 Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu.

11 Akaniambia, Ee, Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neon hili, nilisimama nikitetemeka.

12 Ndipo akaniambia, usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.

13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja, bali, tazama huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

14 Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.

15 Na alipokwisha kusema maneno hayo, nikauelekeza uso wangu chini, nikawa bubu.

16 Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu, ndipo nikafumbua kinywa change nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikusaziwa nguvu.

17 Maana mtumishi wa Bwana wangu huyu atawezaje kusema na Bwana wangu huyu? Kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani, wala pumzi haikusalia ndani yangu.

18 Kisha mmoja mfano wa mwanadamu akanigusa tena, akanitia nguvu.

19 Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope, amani na iwe kwako, na uwe na nguvu, naam!Uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu, kwa maana umenitia nguvu.

20 Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajema, nami nitakapotoka huku, tazama mkuu wa Uyunani atakuja.

21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.

Katika fungu hili la Neno, twapata habari kwamba, maombi yake Danieli yalifika mbinguni.

Mst 12:

“Ndipo akaniambia, usiogope Danieli, kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu na kunyenyekeza mbele zake Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.”

Sala na maombi ya Danieli yalifika mbinguni, yakajibiwa lakini, majibu ya maombi yake yaliyumbayumba angani bila kumfikia, maana yalikwazwa, yakazuiwa na mapepo waovu wa kishetani. Danieli akiwa hali ya wasiwasi malaika Gabrieli kama ilivyo kawaida , malaika Gabrieli, kama ilivyo kawaida, malaika apelekaye jumbe za Mungu Baba, akamtokea Danieli na kumuarifu Danieli haya mambo.

Na katika mstari wa 20 Mungu alimtuma malaika mkuu Mikaeli, msaidizi wa Israeli, akapiga vita majeshi ya pepo wabaya wakaloweka wakashindwa, majibu ya maombi ya Danieli yakamfikia.

Hata wa leo, na ukweli huu waonyeshwa katika Waefeso 2:1-2, twapigana vita vya kiroho na mapepo ya kishetani. Nasoma maneno ya mstari:

1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

Jambo hili na ukweli huu wapaswa kutuweka katika hali tahadhali, katika sala na maombi yetu, maana yupo katika vita vya kiroho. Kila mmoja wetu ahitaji utakaso, tuweze kutembea na Bwana, kwa kulitii

Neno lake Mungu. Tusimame imara katika Neno lake Mungu na maagizo yake. Neno lake Mungu ndilo taa ya miguu yetu, na mwanga wa njia zetu. Lisome na ulikariri Neno, maana vita vya yule mwovu shetani ni kali. Na kama alivyomshinda Yesu, ndivyo tutakavyo shinda kwa Neno lake lililo hai, na kwa damu ya Yesu Kristo msalabani na ushuhuda wa midomo yetu, kwamba tunampenda na kumwamini Mwana Kondoo – Yesu Kristo.

Tukisimama katika ahadi zake Mungu, tutakuwa washindi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!