Wafalme Wamo Mikononi Mwa Mungu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Wafalme Wamo Mikononi Mwa Mungu
Loading
/
Danieli 4:19-27

Natumai kwamba U buheri wa afya msikilizaji. Jina langu ni David Mungai, na leo twalichambua Neno la

Mungu kutoka Danieli 4:19-27 ‘WAFALME WAMO MIKONONI MWA MUNGU’

Hiki ni kipindi cha ‘Matumaini’.

Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena. Leo twalichambua Neno la Mungu kutoka Danieli 4:19-27. Wafalme wamo mikononi mwa Mungu.

Nasoma;

19 ‘Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza akashangaa kwa muda na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao na tafsiri yake iwapate adui zako.

20 Ule mti uliouona, uliokua, ukawa wa nguvu, urefu wake ukavuka mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote

21 Ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote, ambao chini yake Wanyama wa kondeni walikaa na ndege wa angani walikuwa na makao yao Katika matawi yake

22 Ni wewe, Ee mfalme, uliyekua na kupata nguvu, maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia

23 Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi naye ni mtakatifu akishuka kutoka mbinguni akisema, Ukateni mti huu mkauangamize ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi pamoja na pingu ya chuma na shaba: katika majani mororo ya kondeni kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake na iwe pamoja na Wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake

24 Tafsiri yake ni hii, Ee mfalme nayo amri yake Aliye juu iliyomjia bwana wangu, mfalme

25 Ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu na makao yako yatakuwa pamoja na Wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu naye humpa yeye amtakaye awaye yote.

26 Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake, ufalme wako utakuwa imara kwako baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala

27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme shauri langu lipite kibali kwako ukaache dhambi zako kwa kutenda haki ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini, huenda ukapata kuzidishwa siku zako za kukaa raha.

Kutoka kwa jungu hili la Neno la Mungu twapata mafunzo muhimu sana.

Mstari wa 19

‘Ndipo Danieli aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema Ee, Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao na tafsiri yake iwapate adui zako. Nebkadneza, ndiye aliuharibu mji wa Yerusalemu na akamteka Danieli akamfanya mtumwa hatimaye, akampa Danieli kazi ikulu lakini wakati Danieli alipwa ujumbe na Mungu kuhusu hukumu ya Mungu, Danieli alijuta akilini na moyoni mwake, na akapenda sana kumsihi mfalme atubu na ghadhabu ziondolewe. Skiza maneno ya mstari wa 27

Kwa sababu hii, Ee mfalme shauri langu lipate kibali kwako ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.

Kwa maneno hayo hayo ya Danieli kwa mfalme, twawasihi na wale wenye mamlaka nchini.

Ee wakuu wetu katika shughuli za kutuongoza aacha dhambi zako, aacha maovu, wahurumie maskini huenda ukapata kuzidishwa siku zako za kukaa raha, nyumbani na hata kazini mwako. Na hivyo utaiepuka na hukumu ya mungu.

Nasi tulio na ujumbe wa Neno tusiogope kusema kuihubiri na hata kutangaza ukweli na hata hukumu ya Mungu kwa wote wanaowanyanyasa maskini. Na mkumbuke ya kuwa kanisa ndilo sauti ya Mungu.

Tusimame imara na wima tuseme ukweli wa Mungu na Neno lake kama Danieli na ukumbuke ya kwamba Danieli alikuwa mtu wa kumtafuta Mungu kwa maombi na alikuwa na uhusiano mwema tena wa karibu na Mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!