Dhiki Kuu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Dhiki Kuu
Loading
/
Danieli 12:1-13

Hujambo msikilizaji wangu popote ulipo. Karibu tujifunze neno la Mungu pamoja. Hiki ni kipindi cha “MATUMAINI” Leo tunachambua neno la Mungu kutoka Danieli 12:1-13, jina langu ni David Mungai, karibu.

Wimbo, halafu tuendelee.
WIMBO

Karibu tena, tujifunze neno. Danieli 12:1-13

1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemedari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako, na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo, na wakati huo watu wako wataokolewa, kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.

2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele wengine aibu na kudharauliwa milele.

3 Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.

4 Lakini wewe, Ee, Danieli yafunge maneno haya ukakitie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

5 Ndipo mimi, Danieli nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili mmoja ukingoni mwa mto upande huu na mmoja ukingoni mwa mto upande wa pili.

6 Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto. Je, itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu?

7 Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitaru aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapa alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele. Ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.

8 Nami nikasikia, lakini sikuelewa ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?

9 Akasema, enenda zako Danieli maana maneneo haya yamefungwa na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho.

10 Wengi watajitakasa, na kujifanya weupi na kusafika bali wabaya watatenda mabaya, wala hataelewa mtu mbaya awaye yote, bali wao walio na hekima ndio watakaookolewa.

11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakalosimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.

12 Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.

13 Lakini enendo zako hata utakapokuwa mwisho ule, maana wewe utastarehe, nawe utasimama katika kura yako mwisho wa siku hizo.

Katika fungu hili la Neno la Mungu, mst 1-2, twapata funzo la kufufuliwa kwa walio haki wakati wa kurudi kwake Yesu mara ya pili. Kabla ya ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo ili watawale na Bwana Yesu Kristo.

Na mstari wa pili watoa unabii wa kufufuliwa kwa wale waovu baada ya ufalme wake miaka elfu, kama tunavyosoma katika Ufunuo 20:5

Waovu watafufuliwa, ili wahukumiwe kutupwa katika bahari iwakao moto na kiberiti milele. Na hiki ndicho kifo cha pili tunayemwamini Yesu, tutaishi na Yesu milele.

Mst 3 ‘Na walio na hekima, watangaa, yaani, wakati wa dhiki kuu kutakuwepo na waamini shupavu, watakaowaongoza na kuwaonyesha uongo wa MPINGA KRISTO. Watu watakuwa na harakati za kutaka kujua mwisho wa dhiki utakuwa lini. Hata Danieli, hakuelewa na kula jambo katika unabii, kama tunavyosoma katika mstari wa nane ‘Nami nikasikia lakini sikuelewa …’ maneno ya mstari wa 13. Danieli apewa tumaini n mwenyezi Mungu.

Mst 13 ‘Lakini enenda zako hata utakapokuwa mwisho ule, maana wewe utastarehe, nawe utasimama katika kura (allotted portion)

Yako mwisho wa siku hizo’

Kama matumaini makuu kwa yeyote anayemcha Mungu, na kumwamini Yesu, maana ndiye, njia, kweli na uzima.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!