Tutaishi Namna Gani

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Tutaishi Namna Gani
Loading
/
I Wakorintho 5:9-13

Salaam msikilizaji wangu na karibu tujifunze neno la mungu pamoja. Jina langu ni David Mungai. Leo twalichambua neno kutoka 1 WAKORINTHO 5:9-13

Tutaishi Namna gani? Karibu, wimbo kwanza halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena tujifunze neno la Mungu,

Mwalimu mmoja wa theolojia katika chuo kikuu cha Pennsylvania alisema, namna kitabu cha sharia za

Maisha, mazingira ndiyo hutufunza namna ya kuishi

Baadaye aliondoka kutoka Pennsylvania, kwenda Israeli akiwa na kusudi la kuandika vitabu vya Injili- Mathayo, Marko ,Luka na hata Injili ya Yohana lakini akafa katika pori la Yuda. Hata waleo, alikufa namna gani?

Kitabu cha sharia za Maisha tunacho. Biblia na jibu la swali tutaishi namna gani? Jibu lipo katika Biblia.

Nasoma kutoka 1 WAKORINTHO 5:9-13

9 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane kabisa na wazinzi

10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au wenye kutamani au wenye kuabudu sanamu, maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

11 Lakini mambo yalivyo naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi mtu wa namna hii msikubali hata kula naye

12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?

13 Lakini hao walio nje, Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

Twauliza tuishi vipi na wengine ndani ya kanisa na nje?

Katika mstari wa tisa msichangamane yaani kuwa na ushirika wa karibu katika ulimwengu huu ni vigumu kujitenga kabisa na ya ulimwengu katika shughuli zetu za kila siku, kama alivyosema. Paulo katika mstari wa kumi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia au na wenye kutamani, au na wanyanganyi au na wenye kuabudu sanamu maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

Zaidi katika mstari wa 11 paulo alionya kwamba hatuwezi kuwa na ushirika wa karibu na ndugu katika Kristo, aliyeangukia dhambini na amo katika kipindi cha kupewa nidhamu,

Mst 11 wasema,
‘……msichangamne na mtu aitwaye ndugu , akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi mtu wa namna hii, msikubali hata kula naye…’

Kwa kifupi tuwe waangalifu ni nani tunashiriki naye, haswa katika meza ya Bwana. Hata hivyo kanisa laonywa katika mstari wa 12-13. Kunao watu ambao wamekataa kumwamini Yesu Kristo na kumpokea kuwa mwokozi na mkombozi

Mst 12-13

12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hawahukumu hao walio ndani?

13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

Si letu kuwahukumu wenzetu, hata wasioamini, Mungu ndiye atatoa hukumu, letu ni kurekebisha yaliyo ndani ya kanisa na kushughulikia uenezaji wa injili ya wokovu katika Yesu Kristo.

Bado tuko ulimwenguni huu wa taabu na matatizo mengi lakini Yesu alituombea pamoja na mitume.
Injili ya Yohana 17.15-20

15 ‘Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu, bali uwalinde na yule mwovu’

16 Wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu

17 Uwatakase kwa ile kweli neno lako ndiyo kweli

18 Kama vile vilivyonituma mimi ulimwenguni , nami vivyo hivyo naliwatua hao ulimwenguni

19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe ili na hao watakaswe katika kweli

20 Wala si hatotu, ninawaombea lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.

Shangwe na vigelegele kwa Yesu kwa kutuombea hata wa leo, ameketi mkononi mwa Mungu baba bado akituombea.

Ndiye mpaji wa hekima haki, utakaso na ukombozi wa Kristo ndiye ukamilifu wa wokovu wetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!