Kristo Yuhai

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kristo Yuhai
Loading
/
I Wakorintho 15:1-11

Hujambo Na karibu. Leo twalichambua fungu la neon kutoka 1 Wakorintho 15:1-11 ‘KRISTO YU HAI’. Jina langu ni David Mungai Wimbo halafu tuendelee.

Naam karibu tena. Twalichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakorintho 15:1-11 ‘KRISTO YU HAI,’

Tangu jadi watu wengi wamepuuza kufufuka kwake Kristo. Natumia jina hilo ‘kristo’ maa limetafsiriwa kutoka neon la kigiriki ambalo ni sawa na la kiebrania ‘masiya’ maana yake ni ‘aliyetiwa mafuta. Kristo alitulelea huduma maalum ya kuntoende dhambi na kutuokoa tunapotubu dhambi na kumwamini na kumkiri na midomo yetu kuwa ni Bwana.

Mwana wa Mungu, akachukua mwili wa kibinadamu, akazaliwa na Bikira Mariamu. Alisulubiwa msalabani kwa niaba na kwa ajili ya dhambi zetu. Siku ya tatu kafufuka kutoka kwa wafu, na huko ndiko atatoka kuja hapa duniani kulinyakua kanisa lake.

Yesu Kristo yu hai. Nasoma sasa kutoka 1 Wakorintho 15:1-11.

1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,

2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure.

3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara;

6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.

10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

Msikilizaji, kufufuka kwake Yesu Kristo, ni ukweli ambao, kuificha ni vigumu. Wengi wamejaribu lakini hawakuweza, baadhi yao waliaga dunia wakiwa bado wajaribu. Hebu sikiliza tena nikisoma tena fungu hili la Neno, mstari wa kwanza hadi wa nne. 1 Wakorintho 15:1-4

1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,

2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure.

3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.

Neno limeshuhudia na kuweka muhuri, kufa na kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Wayahudi na Wayahuni.

Katika kitabu cha Matendo ya mitume 13:26-35, Paulo aliwahubiria Wayahudi kuhusu kufufuka kwake Yesu, na katika Matendo ya mitume 17:29-31. Paulo aonekana akiwahubiri Wayahuni ukweli huu huu wa kufufuka kwake Yesu Kristo. Ni kweli kabisa Yesu alisubuliwa msalabani, akatuondolea dhambi, akazikwa na siku ya tatu akafufuka.

Na huu ndio msingi wa Injili. Habari njema ya wokovu. Na Zaidi sana-kufunika kwake Kristo kumetia muhuri umuhimu wa Injili, Habari njema iletao wokovu na uzima wa milele, milele na milele.

Kufunika kwake Yesu Kristo, kulishuhudia na waumini Zaidi ya mia tano. Mst 6-8

6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

Kufufuka kwake Yesu Kristo ni Dhahiri na Yesu yu hai, na Zaidi sana, Yu hai maishani mwetu, wote tunamwamini.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!