Sema ukweli

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Sema ukweli
Loading
/
Mwanzo 42:29-38

Hujambo. Leo katika kipindi hiki twalichambua neno kutoka Mwanzo 42:29-38. “Sema ukweli”. Jina langu ni David Mungai. Ukweli ni jambo la kupalilia maishani. Hakuna ampendaye mtu asiyemwaminifu. Twapendezwa sana na wale wanaosema ukweli, na hata wale watu wanaozingatia mambo ya ukweli, kwa sababu Biblia husema ni vibaya kusema uongo. Kwa mkristo ni jambo la muhimu kuishi na ukweli. Mambo huwa rahisi unapoishi na watu wa ukweli. Mambo huwa rahisi unapoishi na watu wa ukweli, lakini kuishi na watu waongo ni jambo ngumu sana. Ujumbe wet wa leo “SEMA UKWELI”. Nasoma kutoka Mwanzo 42:29-38

Wakaja kwa Yakobo, baba yao. Katika nchi ya kanaani wakampasha habari za yote yaliyowapata wakisema, mtu yule aliye bwana wan chi alisema nasi kwa maneno makali akatufanya tu wapelelezi wa nchi. Tukamwambia, Tu watu wa kweli sisi wala si wapelelezi. sisi tu ndugu kumi na wawili wana wa baba yetu. Mmoja hayuko na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo katika nchi ya kanaani. Yule mtu bwana wan chi akatuambia kwa njia hii nitawajua kama ninyi ni watu wa kweli, ndugu yenu mmoja mwacheni huku kwangu kachukueni nataka kwa njaa ya nyumba yenu mwende zenu. Mkanilelee ndugu yenu mdogo. Ndioo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi bali ni watu wa kweli, basi nitawarudishia ndugu yenu nanyi mtafanya biashara katika nchi hii.

Ikawa walipomimina magunia yao kumbe! Bahasha ya fedha ya kila mtu imo katika gunia lake. Nao walipoziona bahasha za fedha zao, wao na baba yao waliogopa. Yabobo baba yao akawaambia mmeniondolea watoto wangu. Yusufu hayuko wala Simeoni hayuo na Benjamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi. Reubeni akamwambia babaye akasema, uwaue wanangu wawili nisipomrudisha kwako. Mtie katika mikono yangu, name nitamrudisha kwako. Akasema, mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa naye amesalia peke yake mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea. Ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.

Katika fungu hili la neno la mungu twapata vitendo kadhaa zinazotuonyesha ya kwamba kusema uongo ni kubaya. Ripoti ya nduguze Yusufu imetuonyesha umuhimu wa kusema ukweli. Waliporudi kutoka misri, walitoa habari yoe hasa kumhusu Yusufu ambaye sasa amekuwa mmoja wa wakuu wan chi ile na vile alivyowachukulia kuwa ni wapelelezi. tulimwambia ukweli lakini alisisitiza kuwa lazima tumpelekee Benjamini apate kutuamini. Alihimiza kwamba tumuache simeoni misri, akae kule mpaka ule wakati atakamowna benjamini. Walipeana habari za kweli, lakini walipofungua magunia yao wakapata pesa ile ile walikuwa wamepewa na baba yao ya kununua nafaka. Wakajawa na hofu na uoga.

Hapo awali ndugu zake walimwuza. Yusufu kama mtumwa wakamchinja mwanambuzi, na kuitumbukiza kanzu lake maridadi ndani ya damu wakampelekea baba yao. Wakisema labda mwanao aliuliwa na mnyama mkali. Hata hivyo Yakobo aliichukua ile habari kutoka misri kuwa ni kweli. Walipeana habari kama ilivyokuwa nchini misri. Jambo la pili ni kwamba, walipoona bahasha za pesa kwa kila gunia la nafaka wote. Baba na wanawe kana kwamba ni mtego kuwapata kama ni watu waminifu na wa kweli, lakini Yakobo hakukubali kwa urahisi kwa sababu Simeoni ameachwa misri, na alikuwa ameamini ya kwamba Yusufu alikuwa ameuliwa na mnyama mkali, sasa wanawe wataka kunchukua Benyamini kitinda mimba wa Yakobo. Akachanganyikiwa hata akasema: Ms 36…mambo haya yote yamenipata mimi”

Reubeni mwanawe wa kwanza akapendekeza “Uwauwe wanangu wawili nisipomrudisha kwako” lakini Yakobo akasema mst 38 “Mwanangu hatashuka pamoja nanyi maana nduguye amekufa naye amesalia peke yake” Yakobo alikuwa bado, hajasahau yale yaliokuwa yametendeka kumhusu Yusufu.

Hatumkashifu Yakobo lakini hakujua ya kwamba janga la nja litaendelea na lazima wangerudi misri kutafuta nafaka ya chakula. Hata hivyo, lazima tuelewe ya kwamba anachopanda mtu ndicho atavuna. Yakobo anavuna aliyomtendea babake. Alimdanganya kuwa yeye ndiye alikuwa Esau. Baba yake akampa mbaraka wa kwanza, badala ya Esau. Akamdanganya babake. Sasa avuna. Amedanganywa kumhusu Yusufu. Akauzwa kama mtumwa Simeoni naye ameachwa misri.

Ni jambo muhimu kwa kila mmoja wetu kusema na kuishi kwa ukweli. Ukiishi kwa ukweli utavuna mema ya ukweli. Ukiwa muongo hutaenda mbali.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!