Uamuzi Mgumu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Uamuzi Mgumu
Loading
/
Mwanzo 42:1-16

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini twaupata “uamuzi magumu”. Mwanzo 43:1-15. Jina langu ni David Mungai. Kila mmoja wetu huamua. Unaamua wakati wa kulala na wakati wa kuamka. Mungu akipenda. Hayo ni maamuzi ya kila siku. Lakini kuamua kuondoka na kuacha nchi yako uende ukaishi ugenini. Huo huwa uamuzi mgumu. Kabla ya uamuzi wa aina hiyo mtu huwa na majibu ya maswali mengi sana.

Nasoma kutoka kitabu cha Mwanzo 43:1-16.

Njaa ikawa nzito katika nchi. Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka misri baba yao akawaambia rudini huko mkatununulie chakula kidogo. Yuda mtu alituagizia sana akisema, hamtaniona. Uso wangu ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi. Ukimpeleka ndungu yetu pamoja nasi tutashuka na kunua chakula. Ila usipompeleka hatushuki maana mtu yule alituambia namtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi.

Israeli akasema mbona mmenitendea vibaya hata mkamwarifu mtu yule ya kwamba mna ndugu mwingine? Wakasema mtu yule alituhoji sana habari zetu na jamaa yetu akisema, Baba yenu angali hai? Mnaye ndugu mwingine? Nasi tukamjibu sawasawa na maswali hayo. Je! Tuliweza kujua ya kwamba atasema shukeni pamoja na ndugu yenu?

Yuda akamwambia Israeli babaye mpeleke kijana pamoja name, tuondoke tuende zetu ili tupate kuishi wala tusife sisi na wewe na watoto wetu. Mimi nitakuwa mdhamini wake umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima. Maana kama hatungalikawia hakika tungaliisha kurudi mara ya pili. Israeli baba yao akawaambia kama ndivyo, fanyeni hivi, twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu mkamchukulie mtu huyo zawadi zeri kidogo na asali kidogo ubani na manemane na jozi na tozi. Mkatwae fedha maradufu mikononi mwenu na fedha zile zilizorudishwa kinywani mwa magunia yenu zirudisheni mikononi mwenu, labda zilisahauliwa.

Mtwaeni ndugu yenu mwondoke na kurudi kwa mtu yule. Mungu mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu mwingine na Benyamini. Name nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa. Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao na Benjamini. Wakaondoka wakashuka mpaka misri wakasimama mbele ya Yusufu. Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao akamwambia msimamizi wa nyumba yake uwalete watu hawa nyumbani ukachinje na kuandalia maana watu hawa watakula pamoja name adhuhuri.

Naam, katika fungu hili la neno la Mungu twapata sababu au mambo kadhaa yaliyomfanya Yakobo kuamua, wanawe kurudi misri. Yakobo au Israeli aliamua kuwaruhusu wanawe kurudi misri kwa sababu palikuwa na janga la njaa. Alisema mst wa 2 “ Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka misri, baba yao akawaambia Ruduni huko mkatununulie chakula kidogo. Lakini yusufu alikuwa amewambia hatuwezi kufanya biashara nanyi msipomleta ndugu yenu mdogo pamoja nanyi msipomleta ndungu yenu mdogo pamoja nanyi Yakobo akawaambia kwani mlimwambia mna ndugu mdogo. Wakamjibu wakamwambia tulimwambia kwa sababu alikuwa ametuuliza maswali yaliyohusu familia yetu. Yakobo akawaruhusu waende pamoja na benjamini.

Jambo la pili ni kwamba. “ mpeleke kijana pamoja name tuondoke tuende zetu, ili tupate kuishi wala tusife sisi na wewe na watoto wetu.

Ikawa ni lazima waende na Benyamini ili wapate kununua chakula. Haya yatukumbusha ya kwamba kunao wakati ambao Esau babake Yakobo karibu atolewe kafara na baba Ibrahimu lakini mungu akamwonyesha kondoo wa kutoa dhabihu. Sasa hapa yakobo anamtoa Benyamini kama kafara ili wapate chakula waishi. Ilikuwa ni wamtoe Benyamini wakikataa wafe njaa. Yalikuwa maamuzi makali. Na hivyo ndivyo Yakobo alimtoa Benjamini ili waokolewe na kifo cha njaa. Zaidi Yakobo alisema wampelekee yule mtu zawadi Zaidi za zeri asali ubani na manemane na jozi na lozi-na kadhalika labda Yusufu angewasikiliza kwa makini. Ni jambo la kupendekeza kuona vile Yakobo aliwafunza watoto wake kunyenyekea.

Lazima tunyenyekee mmoja na mwingine ili tufanikiwe maishani. Lazima tunyenyekee mbele ya mwenyezi mungu ili atukweze kwa wakati wake na kwa njia zake na kwa utukufu wake. Lazima tuwe na unyenyekevu katika familia na shule zetu maana mungu kumpinga mwenye kiburi. Lazima tuwe na unyenyekevu katika familia na shule zetu maana mungu kumpinga mwenye kiburi. Na unyenyekevu ndiyo mwanzo wa safari yetu katika Imani ya ukristo maana hata naye Yesu Kristo aliuacha utukufu wa mbinguni akshuka duniani hii ili kwa kifo chake msalabani kwa Imani tupate wokovu wa roho yetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!