Mungu anasema nini

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu anasema nini
Loading
/
Mwanzo 41:14-24

Hujambo na karibu. Leo katika kipindi cha matumaini twajifunza; Mungu anasema nini? Somo lapatikana kutoka Mwanzo 41:14-24. Mawasiliano huwa nan cha mbili. Mungu amewasiliana nasi kwa Neno lake kwa sabbau ndiye aliyetuumba na Yeye hupendezwa sana anapowasiliana na vyumbe vyake. Neno lake ndilo msingi wa mawasiliano yetu na Mungu. Je, umewahi kuyapokea mawasiliano ya Mungu kwako. Nyakati zingine Mungu huwasiliana nasi katika kweli zinazotukumba. Nyakati zingine kwa ndoto nyakati zingine kwa marafiki wahubiri manabii. Njia za Mungu si kama zetu. Yeye ndiye Mungu Mwenyezi. Nyakati zingine twalia hali ya anga, joto, baridi, matetemeko ya ardhi na kadhalika. Maneno hayo yanikumbusha nyanya. Nyanya yangu alipoona umeme na kusikia sauti ya radi kila wakati alilia kwa sauti “Ngai ndugatunine” Mungu usituangamize. Mungu huwasiliana nasi vyumbe vyake kwa njia nyingi sana. Mungu asema nini sasa. Tusome kitabu cha Mwanzo 41:14-21

“Ndipo Farao akapeleka watu akamwita Yusufu wakamleta upesi. Kutoka gerezani. Akamnyoa akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. Farao akamwambia Yusufu, nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria, nami nimesikia habari zako, ya kwamba usikiapo ndoto, waweza kunitafasiria; nimesikia habari zako, ya kwamba usikiapo ndoto, waweza kuitafsiri. Yusufu akamjibu Farao akisema, Si mimi; Munguatampa Farao majibu ya Amani. Farao akamwambia Yusufu, katika ndoto yangu nalikuwa nikisimama ukingoni mwa mto. Na tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda baada yao, dhaifu wabaya sana wamekonda; katika nchi yote ya Misri sijaona kama hao kwa udhaifu. Na hao ng’ombe waliokonda wabaya, wakawala wale ng’ombe saba wa kwanza wale wanono. Na walipokwisha kuwala haukutambulikana ya kwamba wamewala, bali wakaonekana wabaya kama kwanza. Basi nikaamka, kisha nikaona katika ndoto yangu na tazama masuke saba yanatokeza katika bua moja, mema yamejaa. Na tazama masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki yakatokeza baada yao. Na hayo masuke dhaifu yakameza yale masuke saba mema. Name nikawaambia hao waganga wala hakuna aliyeweza kunionyesha maana yake.”

Katika fungu hili la Neno la Mungu twamwona Mungu akisema na mfalme asiyemcha Mungu, na ningependa tumtizame kwa undani Yusufu na ujuzi wake. Hatua ya kwanza: Yusufu aliitwa. Munyweshaji alikumbuka ya kwamba, Yusufu alimsaidia kutafsiri ndoto yake. Hata akamwita kwa kabila lake mwebrania. Wakamleta Yusufu kwa haraka. Yusufu alionekana mtu wa kipekee. Yusufu aliogeshwa haraka akavalishwa nadhifu, akapelekwa kwa mfalme Farao. Ndipo mfalme akasimulia ndoto yake na akamwambia Yusufu kwamba hakuna aliyeweza kuitafsiri. Ikawa changa moto. Je, Yusufu ataweza? Je, Yusufu alikuwa mwerevu kuliko waganga wote katika nchi ya Misri? Changamoto kweli. Yusufu alijibu akasema: “Si mimi Mungu atampa Farao majibu ya Amani.”

Nchi ya Misri ilijulikana sana kwa elimu ya hali ya juu. Na pia ilijulikana sana kwa uganga na kuabudu miungu yao. Hii ndiyo sababu Yusufu amwambia Farao kwamba chanzo cha hekima yote ni Mungu. Mungu mwenye enzi muumba wa mbingu nan chi, na ndiye Mungu wa Israeli- ndiye mwenye uwezo wote. Yusufu akamkumbusha Farao kwamba kwa huyu Mungu aishiye milele hakuna lisilowezekana. Na ni kwa uwezo wake ndoto zaweza kutafsiriwa. Hatua ya pili. Yusufu aliambiwa. Farao alimwambia Yusufu.

“Farao akamwambia Yusufu, katika ndoto yangu nalikuwa nikisimama ukingoni mwa mto, na tazama ng’ombe saba wanatoka mtoni, wanono wazuri wakajilisha manyasini. Kisha tazama ngombe saba wengine wakapanda baada yao dhaifu wabaya sana wamekonda. Katika nchi yote ya misri sijaona kama hao kwa udhaifu. Nao hao ngombe waliokonda, wabaya wakawala wale ngombe saba wa kwanza wale wanono. Na walipokwisha kuwala haikutambulikana ya kwamba wamewala bali walionekana wabaya kama kwanza. Basi nikaamka. Kisha nikaona katika ndoto na tazama masuke saba yanatokeza katika bua moja, mema yamejaa. Na tazama masuke saba membamba dhaifu wamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Na hayo masuke dhaifu yakameza yale masuke saba mema. Yusufu akamwambia Farao ndoto ya Farao ni moja. Mungu amemwonyesha Farao atakayofanya hivi karibuni wale ngombe saba wema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale ngombe saba dhaifu wabaya waliopanda baada yao ni miaka saba, nay a masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo nilivyomwmabia Farao ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Tazama miaka saba ya shibe inakuja katika nchi yote ya misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya misri na njaa itaiharibu nchi. Ni kwa sababu ya neon hilo Mungu amelithibitisha na mungu atalitimiza upesi. Farao akamwambia Yusufu kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote hapana mwenye akili na hekima kama wewe Basi utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neon lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Tazama nimekuweka juu ua nchi yote ya misri. Mungu anasema: Hekima inayotoka kwake Yeye mwenyewe ndiye chanzo chake n aukijitwalia Mungu mwenyewe atakukweza, heri aliye mnyenyekevu maana Mungu mwenyewe atamkweza.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!