Jiahidi Hujui Ya Kesho

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Jiahidi Hujui Ya Kesho
/
Mwanzo 43:15-25

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha matumaini. Neno la leo twalipata kutoka Mwanzo 43:16-25. Jitahidi maana hujui ya kesho. Jina langu ni David Mungai. Wengi wetu hutamani sana kuyajua ya kesho au ya siku zijazo lakini mungu akaifanya kutowezekana. Ni mwenyezi Mung utu anayajua yote ya siku zijazo. Maisha ya waisraeli na viongozi wao yana mengi ya kutufunza. Walikuwa na changamomoto nyingi maishani na mungu hakuwaachilia. Hebu nisome kitabu cha mwanzo 43:15-25

Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na benjamini wakaondoka, wakashuka mpaka misri, wakasimama mbele ya Yusufu. Naye yusufu alipomwona Benjamini pamoja nao akamwambia msimamizi wa nyumba yake, uwalete watu hawa nyumbani ukachinje na kuandalia maana watu hawa watakula name adhuhuri. Yule mtu akafanya kama yusufu alivyomwambia. Naye akawaleta watu hao nyumbani mwa yusufu.

Lakini watu hao wakaogopa, kwa sababu wameletwa nyumbani mwa yusufu wakasema kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humy, apate kutumeletwa humu apate kutushitaki na kutuangukia atuitwae sisi kuwa watumwa na punda zetu.

Wakamkaribia yule msimamizi wa nyumba ya yusufu wakasema naye mlangoni pa nyumba. Wakamwambia Tazama bwana kweli tulishuka mara ya kwanza, ili tununue chakula. Ikawa tulipofika nyumba ya wageni tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake fedha zetu kwa uzani wake kamili nasi tumezileta tena mikononi mwetu.

Nasi tumeleta fedha nyinginge mikononi mwetu ili tununue chakula. Hatujui ni nani aliyezitia fedha zetu katika magunia yetu. Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope mungu wenu, msiogope, mungu wenu naye ni mungu wa baba yenu amewapa akiba katika magunia yenu. Fedha zenu ziliwasilia kisha akawatolea simeoni. Mtu yule akawaleta wale watu nyumbani mwa yusufu akawapa maji wakatawadha miguu akawapa punda zao chakula. Wakaiweka tayari ile zawadi hata atakapokuja yusufu. Adhuhuri maana wamesikia ya kwamba watakula chakula huko.

Katika fungu hili la neno la mungu Mwanzo 43:15-25 twapata maneno mawili ya busara yanayoweza kuwa msaada kwetu, hasa tunapopatwa na changamoto za siku zijajo. Wanaume wale walioshuka kwenda misri walikuwa ndugu zake yusufu. Walitoka kanaani kwenda misri kununua chakula. Na hii ilikuwa ni baada ya mazungumzo makali na baba yao yakobo. Yusufu alikuwa amewambia hapo awali wasirudi wasipomleta benjamini ndugu yao mdogo. Yusufu alipomwona benh=jamini alimwambia msimamizi wa nyumba yake. “Uwalete watu hawa nyumbani ukachinje na kuandalia maana watu hawa watakula pamoja name adhuhuri.” Ndugu zake Yusufu bado walikuwa na hofu. Yusufu atawafanyia nini. Walikuwa wamechanganyikiwa.

Walidhani kwamba watafanywa watumwa nchini. Misri hawakujua ni nini kingetokea lakini msimamimizi wa nyumba ya yusufu akawatia nguvu na kuwafariji. “Amani iwe kwenu msiogope, mungu wenu naye ni mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu, fedha zenu ziliwasilia..”

Amani iwe kwenu ni maneno ya busara kweli na kutia moyo. Yamkini yusufu alikuwa amezungumza na huyu msimamizi maneno ya mungu wa Israeli. Na huyu ndiye mungu wa Israeli na ndiye mungu wetu katika Yesu Kristo. Huu ni ukweli wa ajabu ni lazima tuukumbuke na tuutilie maanani ya kwamba ya kale, yakiunganishwa na yajayo, jawabu ni la leo. Haya yamaanisha nini? Hayo yamaanisha kwamba ikiwa mungu alikuweka duniani hii na amekulinda kwa nguvu na uweza wake basi na hata katika siku zijazo atafanya hay ohayo maana daima ni mwaminifu, n ahata siku ya leo anao uweza wa kukusaidia na kukupatia riziki. Mungu wetu ndiye juzi jana na leo hata milele. Na twaweza kusema yeye ndiye Ebenezar. Hata sasa BWANA ametusidia-na milele ndiye atatusaidia. Amani iwe kwako. Usiogope.