Rais Alipoomba

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Rais Alipoomba
Loading
/
Danieli 6:10-24

Salaam, msikilizaji wa kipindi cha matumaini. Jina langu ni David Mungai na karibu tujifunze Neno pamoja. Leo twalichambua fungu la Neno kutoka chuo cha Nabii Danieli 6: 10-24: “Rais aliomba.”

Tusikilize wimbo kwanza halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena, tujifunze neno pamoja. Leo twalichambua Neno kutoka Chuo cha Nabii Danieli 6:10-24. Nasema:

10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake ( na madirisha katika chumba chake yaliyokuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu, wake kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

12 Ndipo wakakaribia wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mafalme, Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awayeyote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee, mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo Sheila ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.

13 Basi wakajibu, wakasema, mbele ya mfalme; Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hawakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.

14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana akakaza moyo wake ili kumponya Danieli akastajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.

15 Ndipo watu wale wakakusanyika mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sharia ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lilio marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.

16 Basi, mfalme akatoa amri nao wakamleta Danieli wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.

17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu, naye mfalme kalitia muhuri, kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.

18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake, na usingizi wake ukampaa.

19 Asubuhi, mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.

20 Naye alipokaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akamwambia Danieli, ‘Ee, Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako unayetumikia daima aweza kukuponya na simba hawa?

21 Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi mlele.

22 Mungu wangu ametuma malaika wake naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana si kuwa sina hatia, tena mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno!

23 Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu, wala dhara, halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.

24 Mfalme akaamuru nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli wakawatupa katika tundu la simba, wao na watoto wao, na wale wake zao na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.

Danieli aliokolewa na Mungu. Ni hivi, yatupasa, kuyatarajia makuubwa kutoka kwa mwenyezi mungu.

Hakuna lisilowezekana kwa mungu, msikilizaji. Pamoja na hayo, twajua ukweli kwamba, ‘ sala na dua hayageuza na kuyabadilisha mambo kulingana na mapenzi ya Mungu.

Mlimani Karmeli, Eliya aliomba, moto ukatoka mbinguni ukayachoma madhabahu.

Katika mji wa Filipi, Paulo alitupwa ndani ya jela, akafungwa kabissa. Paulo na Sila, waliomba panapo usiku wa manane, Mungu akawafungulia na kutoka fungu hili la Neno kutoka kitabu cha Nabii Danieli, mfalme aliomba mfalme ambaye alikuwa mtu wa mataifa, akamsujudu Mungu, na akanena uwezo wa

Mungu wetu, Mulumba wa mbingu na nchi. Mungu ana uwezo, na nguvu zote ,na anaweza kuamuru vyumbe vyake hata simba kuyatimiza mapenzi yake. Tusilidhihaki jina tukufu la mwenyezi Mungu.

Danieli pia, alijua siri. Kama ilivyo, kwa Wayahudi kumwomba mungu wakielekeza nyuso zao Yerusalemu, aliomba mara tatu kila siku, na alikataa kabisa kuabudu na kunyenyekea miungu mingine ya sanamu. Alinyenyekea, mbele ya Mwenyezi Mungu na Mungu akamlinda asitatruliwe na simba waliokuwa ndani ya lile tundu. Mungu wetu ana uwezo kuliko uchawi wote kupiga ramli, n ahata zile itkadi kali.

Mungu ana uwezo wa kujibu maombi yetu, kufuatana na kulingana na mapenzi yake. Yu heri Mkristo yule, anazo bidi kuomba. Haijalishi hata ukiwa peke yako kama Danieli. Tukifunze kumwomba Mungu kama Danieli sala na maombi liwe jambo la kawaida, kila wakati, kila siku.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!