Njia Bora Zaidi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Njia Bora Zaidi
Loading
/
I Wakorintho 13:1-13

Hujambo na karibu tujifunze Neno la Mungu pamoja. 1 Wakor. 13:1-3 “NJIA BORA ZAIDI.” Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee kujifunza.

Naam. Karibu tena tujifunze pamoja 1 Wakor. 13:1-13. “NJIA BORA ZAIDI”. Hii ni sura inayofundisha mengi kuhusu upendo. Kunao upendo aina tofauti.

Kunao upendo kutoka neno la kigiriki “Eros” ambao ni upendo kati ya mwanamume na mwanamke uhusiano katika mahaba. Kunao upendo ambao huunganisha maneno mawili ya kigiriki ‘Filos’ na linguine ni ‘adeltos.’ Filos maana yake, upendo wa kifamilia nalo neno “Philadelphia,” mji mmoja katika nchi ya Amerika, maana yake, upendo wa kindugu. Nikimpenda ndugu yangu anayenifuata upendo wa aina hiyo ni Filos.

Kunao upendo wa aina nyingine Agape. Neno linguine la kigiriki. Na upendo huo umeelezwa katika Injili ya Yohana 3:16.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. Neno ‘agape’ lamaanisha, upendo uliopo, hauchoki na hauachi kupenda na hauhitaji malipo. Na huu ndio upendo unaelezwa katika 1 Yohana 4:19.

“Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.” Na Waraka wa Paulo kwa Warumi 5:7-8.

“Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki, lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha, pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Basi sasa tutazame Neno hili la upendo, kutoka 1 Wakor. Sura ya 13. Maelezo ya upendo wa Mungu. Nasoma.

1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua, siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Kuanzia mstari wa tatu, sikiliza kwa makini maana maneno ya mistari hii, yaonyesha upendo ni nini na namna ya kuutumikisha. Baada ya kusoma, fungu hili, ni wimbo, halafu anwani maana ya neno hili lajieleza kinaga-ubaga.

Mst 3. “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikitoa mwili wangu niungue moto kama sina upendo hainifaidii kitu.

4 Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu, upendo hautakabari,haujivuni

5 haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya,

6 haufurahi udhalimu, (kuanzia hapa lugha yabadilika, na kuonyesha yatupasayo kufanya.) haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja pamoja na kweli,

7 huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wowote, bali ukiwapo unabii, utabatilika, zikiwapo lugha, zitakoma, yakiwepo maarifa. Kwa maana tunfahamu kwa sehemu, na tunfanya unabii kwa sehemu, lakini ijapo ile iliyo kamili iliyo kwa sehemu itabatilika.

11 Nilipokuwa motto mchanga nalifahamu kama motto mchanga, tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo, wakati ule tutaona uso kwa uso, wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi name ninavyojuliwa sana.

13 Basi sasa inadumu imani tumaini upendo haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Ninapoyatafakari ya fungu hili, namkumbuka Musa, alipokuwa machungani alipokiona kijiti kiliwaka moto lakini hakikuteketea, Bwana akamwambia Musa.

Kutoka 3:5 “Usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni mwako maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.”

Yaani upendo wa namna hii wapatikana tu kutoka kwa Mungu. Upendo kama huo wapatikana tu kwa uongozi wa Roho mtakatifu. Naye Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu, hawezi kufanya kazi na dhambi, kwa ni muhimu na ni jambo la maana, kutubu, na kuungama dhambi na kumpa Roho wa Mungu afanye kazi ndani yetu na kututumikisha tupate kuzaa tunda la Roho ambalo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole kiasi.

Upendo husawazisha mambo yote. “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.

Mst. 2 “Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.”

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!