Je Kila Mtu Akubalika Kamisani

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Je Kila Mtu Akubalika Kamisani
/
I Wakorintho 5:1-8

Salaam msikilizaji wangu popote ulipo. Karibu tujifunze Neno pamoja kutoka 1 Wakorintho 5:1-8 “Je, kila mtu akubalika kanisani?” Jina langu ni David Mungai. Karibu, wimbo halafu tuendelee kujifunza.

WIMBO

Naam. Karibu tena.

Makanisa mengi, huwakaribisha watu, vizuri sana, kwa nderemo, nduru na makofi hata ya kilo. Kanisa la Korintho lilikuwa hivyo kama tunavyosoma katika .

Kanisa, waumini wote wanaomwamini Yesu, twahitaji usafi. Kanisa la Mungu liwekwe safi. Kanisa lahita kumchukulia hatua, yeyote anayelichafua kwa vitendo vyake. Lazima tuwe macho, na kuchukulia hatua wote waliochafua bila mapendeleo.

Hagai 1:8

Makanisa yahitaji kutakaswa. Twapaswa kucukua hatua ya mapema tunapohisi kwamba twateleza na kwa tahadhari kuwakaribisha wote, tukiyazingatia kanuni za Neno la Mungu.

Nasoma fungu la Neno. 1 Wakor 5:1-8

1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;

5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

6 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?

7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.”

Katika kanisa la Korintho, habari ilikuwa imeenea kwamba, kulikuwa na mtu alikuwa na mke wa baba yake, na Wakristo walikuwa wakijivunia jambo hilo, na hawakusikitika yule mtu aondolewe kanisani.

Wangemwondoa mtu huyo katika orodha ya waumini. Hata kwa watu wale wasilolijua Neno jambo na tabia hiyo haikubaliki. Ni dhambi na ni makosa.

Katika nchi mojawapo ya magharibi katika shirika moja, mchungaji wa makamu, mkewe aliaga na kwa sababu huduma ya uchungaji alianza kutafuta mpenzi mwingine wa kuoa. Akaanza kumtongoza mama mjane kanisani na kutamani uhusiano wa kina ukamilike kabla ya kufunga ndoa. Kanisa liliingilia jambo hilo kwa haraka, nikamwachisha yule mchungaji huduma akawa kama mshiriki wa kawaida.

Kanisa la Bwana wetu Yesu Kristo liwalo lo lote, lazima liwe macho , liwe imara kukabiliana na ye yote anayetaka kulichafua. Zinaa ni dhambi ambayo kweli imewaangusha wengi, na imekatazwa kabisa katika Neno la Mungu.

Tusome mambo ya Walawi 18:8 “…. Usitwae mwanamke pamoja na nduguye (J.Keen) awe mtesi (step mother), na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa uhai.”

Kumbukumbu la Torati 22:22 “Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.”

Katika 1 Wakor 5:2 twapata Neno “Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.”

Na mstari wa tano, waongeza: 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.” Kujisifu kwenu si kuzuri.

Mtu kama huyo achukuliwe hatua ya nidhamu aondolewe aende katika utawala wa shetani, asije akawa na tabia hiyo ya uzinzi na usherati kanisani. Na hiyo tabia mara nyingi uangamizaji n ahata kifo, kama tunavyosoma kutoka 1 Wakor 11:30 Paulo arudia. “Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala(Wamekufa).”

Hii ni tabia mbaya: Sikiliza na usikie nikisoma kutoka 1 Yohana 5:17 “…. Iko dhambi iliyo ya mauti.”
Neno latoa jibu 1 Wakor 5:7 “Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.”

Neno hilo chachu limetajwa pia katika injili ya Mathayo 13:33

Chachu ukiwekwa katika unga wa mandazi-mahamri, chachu haionekani na macho lakini ipo.

Wawezakusema haimo dhami kanisani au maishani mwako, lakini ipo, maana usipoua, wawachukia ndugu na baadhi ya akina dada, wamwonea wivu.. kiburi ndani ya mtu… chachu ya dhambi imo ndani yetu na kati yetu kanisani.

Toba, na kuungama dhambi, ni muhimu na ni lazima maana ingawa twamwamini Yesu, sisi tumesamehea dhambi, lakini bado tupo katika miili hii ya dhambi. Dhambi husababisha kifo na tukisema ya kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe , lakini tukitubu na kuungama Mungu hutusamehe lakini tusiwe na mazoea ya kujumuika katika dhambi.