Jitwalie Ushindi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Jitwalie Ushindi
Loading
/
I Wakorintho 10:1-13

Msikilizaji wangu ni furaha yangu kukukaribisha, katika kipindi hiki, tujifunze Neno pamoja. Jina langu ni David Mungai. Leo twalitazama Neno kutoka I Wakorintho 10: 1-13. “ Jitwalie ushindi. Wimbo halafu tuendelee. Usibadilishe mtamko.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Twalitazama Neno kutoka I Wakorintho 10:1-13. Jitwalie ushindi.

Changamoto maishani zimetuzingira. Fedha hamna. Nafasi za kazi/ajira hazipo. Shughuli za kifamilia zatubana sana. Usingizi hamna. Raha na wako wa karibu hamna. Lakini kati ya mambo hayo yote twawezaje kupata ushindi; na ni lini tutaupata?

Nasoma fungu hili la Neno. I Wakor 10:1-13. Nasoma.

1 Kwa maana, ndugu zangu sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari.

2 Wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari.

3 Wote wakala chakula kile kile cha roho,

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho, kwa maana waliunywea mwamba war oho uliowafuata, na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao, maana waliangamizwa jangwani.

6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

7 Wala msiwe waabudu-sanamu, kama wengine wao walivyokuwa kama iliyoandikwa, watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

9 Wala tusimjaribu Bwana kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10 Wala misnung’unike, kama wengine wao wallivyonung’unika, wakaharibiwa na Mharabu.

11 Basi mambo hayo yaliwapa wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo, anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.

13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu, ila Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo lakini pamoja na lile jaribu, atafanya na mlango wa kutokea ili mweze kustahimili.

Katika fungu hili la Neno, limetueleza vizuri, vile tunavyoweza kupata ushindi maishani yam cha Mungu.

Paulo atumia mfano wa Waisraeli, ambao kama sisi tulivyo, humkosea Mungu na kutenda dhambi. Ndiyo sababu atumia neno “baba zetu” yaani Waisraeli waliounganishwa na Musa kiongozi wao, mst 2 “…wote wakabatizwa wawe na Musa, katika wingu na katika bahari. Wakapewa chakula cha kiroho, na wakanywa maji kutoka jiwe la kiroho. Paulo asema kwamba hilo jiwe ni mfano wa Yesu Kristo, aliyekuwa na Waisraeli, kila wakati. Walipopata shida kama ilivyo desturi ya mwanadamu, waliyakumbuka maisha ya Misri, wakamkasirisha Mungu walipojitengenea sanamu ya ndama, wakaiabudu. Wakamkasirisha Mungu na katika kitabu cha Hesabu 25:9, twasoma kwamba watu 23,000 waliuawa kwa siku. Na wengine wengi waliuawa baadaye. Na wengine wao wakanung’unika.

Lile wingu na mwali wa moto usiku. Zote mbili zaonyesha ya kwamba Kristo alikuwa pamoja na Waisraeli, na kila wakati akawa mlango wa kutokea.

Mst 13. “Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu ila Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea ili mweze kustahimili.

Huo mlango wa kutokea ni uwepo wa Yesu moyoni na maishani mwako. Mwamini Yesu Kristo moyoni mwako, maana ndiye mlango wa kutokea, ndiye atakayekuwezesha kuyastahimili majaribu maishani. Na hivyo ndivyo unavyoweza kujitwalia ushindi maishani.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!