Mkristo Na Dunia

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Mkristo Na Dunia
/
I Wakorintho 3:18-23

Hujambo na Karibu. Leo twalichambua fungu la neno kutoka 1 Wakorintho 3:18-23. Mkristo na mambo ya Dunia. Jina langu ni David Mungai Karibu, wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam. Karibu tena tujifunze neno la Mungu pamoja. Msikilizaji waonaje mambo ya Dunia? Au ulimwengu? Ni wazi kwamba akili za binadamu haziwezi kuelewa au kueleza yote ya ulimwengu.

Katika kitabu cha Mwanzo 15:5 Ibrahimu alikuwa na shaka ya vile uzao wake ungeongezeka duniani kote. Mungu akamwambia;

“…Akamleta nje akasema, Tazama, sasa Mbinguni, kazihesabu…Akamwambia, ndivyo utakavyokuwa uzao wako” mastari wa 16.

Mstari wa 6 “Akamwamini Bwana naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. Ibrahimu hangeweza kuhesabu nyota zote angani, Lakini aliamini.

Mfalme Daudi pia alijishusha kwa unyenyekevu kwa aliyoyaona kama tunavyosoma kutoka Zaburi 8:3

“Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha, mtu ni kitu gani hata amkumbuke na binadamu hata umwangalie?

Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu. Umemuika taji ya utukufu na heshima.

umemtawaza juu ya kazi za mikono yako. Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Kondoo na ng’ombe wote pia, naam, na wanyama wa kondeni.

Ndege wa angani, na samaki wa baharini, na kila kipitacho njia za baharini

Wewe Mungu, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu Jina Lako duniani mwote!

Nabii Isaya naye akasema:

Isayo 40:12-14 “ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake , na kuzikadiri mbingu kwa shubiri na kuyashika mauumbi ya Dunia katika peshi na kuipima milima kwa auzani, na vilima kama kwa mizani?

Ni nani aliyemwongoza roho ya Bwana na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?

Alifanya Shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza maarifa na kumwonyesha njia ya fahamu?
Sasa swali ni hili, huyu Mungu ni nani? Amenya nini? Mtume Paulo ana Neno;

1 Wakorintho 3:18-23; “Mtu asijidanganye mwenyewe, kama mtu akijiona kuwa hekima miongoni mwenu katika dunia hii na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima

Maana hekima ya Dunia hii ni upuzi mbele za Mungu kwa maana imeandikwa, yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao

20 Na tena, bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili

Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu

kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au Dunia au uzima au mauti au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo, vyote ni vyenu

nanyi ni wakristo, na Kristo ni wa Mungu”

Msikilizaji, mtu asijidanganye mwenyewe, kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika Dunia hii na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye Hekima.

Hekima ya Dunia hii ni upuzi mbele za Mungu, kwa sababu, ni Mungu ayajuaye mawazo yetu na hekima yetu, ni upuzi mbele ya Mungu.

Hekima ya Dunia, ni kama sumu ya kujimaliza. Paulo aeleza wazo hilo kwa maneno haya; Warumi 1:18-21; “kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka Mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli na uovu.

kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao kwa maana Mungu amewaridhishia

kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana na kufahamika kwa kazi yake yaani uweza wake wa milele na Uungu wake, hata wasiwe na udhuru.

kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wa kumshukuru, bali walipotea katika uzushi wao na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.

1 Wakorintho 3:21 “Basi mtu ye yote na asijisifie wanadamu kwa maana vyote ni vyenu

22 kwamba ni Paulo au Apolo au Kefa au Dunia au uzima, au mauti au vilivyopo sasa au vile vitakavyokuwapo, vyote ni vyenu

23 nanyi ni wakristo, na Kristo ni wa Mungu.

Njia ni moja- kumwamini na kumjua Yesu Kristo. Na heri anayemchagua Yesu kuwa Mwokozi na Bwana wa maisha yake.

Na ni hekima ya hali ya juu sana, kujua na kufahamu ukweli kuwa sisi ni mali yake Yesu, na warithi pamoja naye Mbinguni.

Muache Mungu awe Mungu maishani mwako/ Mwetu, na utashangaa kujua ya kwamba yote ni yetu katika Kristo