Nidhamu Maishani

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Nidhamu Maishani
Loading
/
I Wakorintho 4:16-21

Hujambo mimi naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha kulichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakorintho 4:16-21 “Nidhamu maishani.”

Karibu wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Biblia yaonyesha wazi ya kwamba twahitaji nidhamu maishani. Kwa sababu zifuatavyo.

(1) Neno limesema, katika Waraka wa Paulo kwa Warumi 3:9-18 “Hakuna mwenye haki hata mmoja.. Hakuna afahamuye, Hkuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wiote pia. Hakuna mtenda mema, la, hata mmoja, kumcha Mungu hakupo machoni pao.”

Hivyo ndivyo tulivyo – kila mmoja wetu.

Hata hivyo twahitaji nidhamu maishani, maana, hata kama tumeokoka, utu wetu wa kale bado uko ndani yetu. Na tamaa za mwili na za dunia zatunyemelea kila wakati.

Katika waraka wa Paulo kwa Warumi Paulo atukumbusha Warumi 7:14-20

14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.

17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.”

Mstari 25: “Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

Naam. Hivyo ndivyo tulivyo tu wenye dhambi waliohurumiwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Bado tuko katika miili hii ya dhambi.

Ni miito na mvuto ni mingi ya tamaa na kimwili na tamaa za dunia n ahata shetani atutafuta kama simba akitafuta mawindo yake ameze. Na hali hii yaonyesha ya kwamba twahitaji nidhamu maishani. Nasoma sasa kutoka 1 Wakor 4:16-21

16 Basi, nawasihi mnifuate mimi.

17 Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.

18 Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.

19 Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao.

20 Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.

21 Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?”

Katika maneno ya mstari wa 16 na 17, Paula awaambia Wakristo wa Korintho, wamuige yeye. “Basi nawasihi mnifuate, kama mnavyomfuata Kristo. 1 Wakor 11:1 “Mnitafute mimi kama mimi mnavyomfuata Kristo.”

Paula katika pilka pilka zake za kuhubiri Injili katika safari yake ya pili, alifika Derbe, akampata kijan Timeotheo mama yake alikuwa Myahudi na baba Myunani. Akampenda Timotheo akamfunza mengi ya Kristo. Paulo alimfunza mengi kumhusu Kristo. Kijana naye akaimarika kiroho, na hata kutahiriwa na Paulo.

Hapa basi twaona ya kwamba, Paulo amtuma Timotheo kwa kanisa la Korintho kwa ujumbe huu.
Mstari 16-17 “Basi, nawasihi mnifuate mimi. 17 Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo.”

Timotheo alitumika na Paulo kwa uangalifu sana. Alijitolea sana. Paulo alimfunza Timotheo Neno bila kukoma na kwa unyenyekevu na kumwelekeza kwa Kristo. Maisha yao, Paulo na Timotheo yaliwavuta wengi kwa Kristo. Hawakuwa na lengo linguine la kumtukuza Yesu Kristo. Na hii ndiyo sababu aliwashauri Wakorintho wauige mfano wake wac kumfuata Kristo na ukweli wa Neno.

Si dini, si sifa, si elimu, balin wawe na nidhamu ya kumfuata na kumhubiri Kristo peke yake na kuhudumu na Wakristo wengine, kwa nidhamu ya kumfuata Yesu Kristo, kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Mstari wa 20-21

20 Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.

21 Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?”

Ufalme wa Mungu si kwa Neno tu bali ni nguvu. Si maneno tu bali ni nguvu ya kubadilisha maisha ya kila anayemwamini Kristo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!