Kuamini Ni Lazima

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kuamini Ni Lazima
/
I Wakorintho 15:20-28

Hujambo msikilizaji. Jina langu ni David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha “MATUMAINI”. Tujifunze Neno la Mungu pamoja. 1 Wakor. 15: 20-28 ,“ KUAMINI NI LAZIMA”. Karibu wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena tujifunze Neno Kutoka 1 Wakor. 15: 20-28 ,“ KUAMINI NI LAZIMA”. Kwa sababu hatuna ushihidi mwingine wa kufufuka kwake Yesu, ila kaburi tupu basi twategemea Imani yetu kwamba Yesu alifufuka. Twaamini ya kwamba kulingana na vile tunasoma katika Bibilia Bwana wetu Yesu Kristo alifufuka kwa ushindi mkuu. Lazima tuuamini ukweli huu. Nasoma sasa fungu hili la Neno.

1 Wakorintho 15:20-28

20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu limbuko lao waliolala.

21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika, na kiyama ya watu ililetwa na mtu.

22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

23 Lakini kila mmoja mahali pake, limbuko ni Kristo baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

24 Hapo ndipo mwisho atakapompa Mungu, Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wake wote na mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye hata awaweke maadui wake chini ya miguu yake.

26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, vyote vimetiishwa, ni Dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayuma.

28 Basi vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake ndipo mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba mungu awe yote katika wote.

Kutoka kwa fungu hili la Neno la Mungu, katika mstari wa 22 twapata maneno, “ … katika Kristo wote watahuishwa” na hii yamaanisha ya kwamba Wakristo tutafufulkiwa, kuhuishwa, kupewa miili mipya.

Pamoja na hayo, kuanzia mstari wa 23-24, twapata maneno yanayotuonyesha utaratibu wa fufuo.
Kwanza kabisa ni ufufuo wa Bwana wetu Yesu Kristo; pili kufufuliwa kwa Wakristo, wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa. Kama tunavyosoma katika 1 Wathesalonike 4:13-18. Tusome.

13 Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.

14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.

15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala, mauti.

16 Kwa sababu bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao, katika mawingu, ili kumlaki Bwana hewani, na hivyo tutakuwa na Bwana milele.

18 Basi tarijianeni kwa maneno hayo.

Na ufufuo wa mwisho, utakuwa mwishoni mwa itawala wake Yesu Kristo wa miaka elfu; kama tunavyosoma katika Injili ya Yohana 5:28-29

“Msistaajabie maneno haya; kwa maana saa yayo ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

Kwa hiyo ni muhimu kumwamini Yesu Kristo maana, ndiyo njia pekee ya kuingia mbinguni, na kuishi na Bwana wetu Yesu Kristo milele. Hakuna hukumu ya adhabu tena. Mna ufufuo na uzima wa milele katika Yesu.