Linda Maisha Yako

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Linda Maisha Yako
Loading
/
I Wakorintho 8:1-13

Hujambo na karibu tujifunze neno pamoja. Leo twalitazama kwa undani fungu la neno kutoka I Wakorintho 8:1-13 linda Maisha yako. Jina langu ni David Mungai.

Karibu, wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena, tujifunze neno pamoja I Wakorintho 8:1-13

Katika na wakati PAULO aliwaandikia wakorintho waraka huu, kulikuweko na watu waliowatolea kafara miungu yao, halafu nyama iliyobaki iliulizwa sokoni. Paulo hapa awaonyesha wakristo namna ya kujilinda katika mambo hayo.

Nasoma sasa

1 na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi.ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.

2 mtu akidhani ya kuwa anajua neno hajui neno lolote bado, kama impasavyo kujua

3 lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye

4 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu na kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.

5 kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu ama mbinguni ama duniani kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi

6 lakini kwetu sisi mungu ni mmoja tu, aliye baba ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake yuko na bwana mmoja Yesu Kristo ambaye kwake vitu vyote vimekuwepo na sisi kwa yeye huyo

7 bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote, ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa huwa kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu hunajisika

8 Lakini chakula hakituhudhurishi (commend us) mbele za Mungu, maana tusipokula hatupunguziwi kitu wala tukila hatuongezewi kitu

9 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.

10 Kwa maana mtu akikuona wewe uliye na ujuzi umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?

11 na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake

12 Hivyo mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu mnamtenda dhambi Kristo

13 kwa hiyo, chakula kikimkaza ndugu yangu hakika sitakula nyama hata milele nisije nikamkwaza ndugu yangu.

Twamjua Mungu mmoja, muumba wa mbingu nan chi, baba wa bwana wetu YESU KRISTO na ndiye baba wetu- na katika neno hili la Mungu mst wa 4 na 5, Paulo akatoa kuwa hakuna kitu kama sanamu, lakini kuna miungu mingine ambayo tuliipa nafasi yaweza kututawala vibaya,

Wakorintho, kama tulivyo walipenda nyama choma sana. Kwa hiyo hata nyama za madhabahu ya miungu yao, na hivyo waliwakwaza watu hata wakristo waliokuwa wachanga na wadhaifu kiimani

Sikuliza maneno ya mstari wa 12 tena

Hivyo mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu mnamtenda dhambi Kristo.

Mwenye sikio na asikie ya kwamba unapomtenda unapomjeruhi mtu katika dhamiri yake, wamemtenda dhambi KRISTO. Ndugu au dada katika Kristo ni mboni la jicho. Tuwe tahadhari tusiwakwaze wenzetu.

Na hii ndiyo sababu Paulo amesema katika mstari wa 13,

Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.

Hapa basi twapata kanuni ya kutuongoza katika uhusiano wetu na wakristo wengine nyumbani kazini n ahata kanisani

Hakuzingatia mambo yake mwenyewe binafsi asiwakwaze ma kuwapotosha walio wadhaifu katika Imani moyo na Maisha yako ni muhimu nay a dhamani kubwa, milele na milele machoni mwake Mungu.

Nyama choma, na kuku choma, natutaziacha hapa hapa, twende kwetu mbinguni kuishi na kukaa na bwana wetu Yesu kristo.

Kumbuka Maisha yetu ni kama hema.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!