Maisha Ya Ndoa

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Maisha Ya Ndoa
Loading
/
I Wakorintho 7:1-9

Hujambo msikilizaji. Karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakorintho 7:1-9. “MAISHA YA NDOA.” Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Karibu tena,, Paulo, ktikla fungu hili la Neno la Mungu, 1 Wakorintho 7:1-9, aeleza , namna tunavyoweza kuishi Maisha ya Ndoia.

Nasoma: 1 Wakorintho 7:1-9.

1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.

2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.

5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

6 Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.

7 Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.

Katika fungu hili la Neno, Paulo awajibu Wakristo wa kanisa la Korintho- Awajibu maswali waliokuwa wamemuuliza kuhusu ndoa. Ndoa ni muhimu katika kanisa, maana uhusiano mwema hujenga kanisa na uhusiano mbaya hubomoa.

Maneno ya mstari wa kwanza yaomyesha wai, kwamba wakorintho walikuwa wamempelekea Paulo, barua iliyokuwa na maswali ya ndoa.

Mst1. “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika.”

Yanaonekana kwamba Paulo alipendekeza Maisha ya kutooa, lakini mtu aishi kwa adabu la sivyo mtu aoe au aolewe.

Mwanaume asimguse mwanamke kama hataki kumwoa, ukifanya hivyo, wazidisha uovu. Msichana au mke au mume wa mtu ni moto wa kuotea mbali. Na ukianza mchezo huo ghadhabu ni nyingi, tena za kudumu, vigumju kusahau. Acha mchezo huo bwana utakumaliza ni shimo halina mwisho wake, ni kaburi ambalo limezikwa wengi, tukiwaona na macho yetu.

Ili kuondoa hatari hii na kwa sababu ya zinaa, basi oa au uolewe.

Lakini hata baada ya wawili kuwa nasema wawili mwanamke na mwanamume ni muhimu kuheshimu ndoa yen una kuondoa nyavu za bui. Zinazokwaza uhusiano wenu katika ndoa. Kwa mfano Mst 5:

“Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.”

Yamkini nasema na mume au mke aliye katika ndoa. Neno ni hilo “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda (mkubaliane.) tutakaa siku kadhaa, tuombe au tushukuru halafu mambo yarudi hali ya kawaida.

Na ili mfurahie uhusiano huu wa ndoa, kila mmoja na awajibike vilivyo. Pamoja na kumwombea mpenzi wako, ni vyema ujitayarishe kumpokea.

Kumbuka siku zile za mwanzo, mwanzo wa uhusiano wenu. Simu ziikuwa zimefunguliwa, si mteja: maneno nayo na kutembeleana na kuvalia ulivalia nadhifu kampokee wenzako. Ukijua yu karibu kurudi, jitayarishe kumpokea, kama kuna mbwa, wewe na huyo mbwa muwe wa kwanza kumlaki pale kwenye lango. Kopo la uji au kikombe cha chai tayari, msaidie kubeba kilicho mkononi, koti lake, kwa wardrobe, kabla ya kwenda kulala mshwaki mdomoni oga, na kadhalika, muwe safi, hiyo ndiyo njia na mbinu ya kufurahia yatakayofuata. Kama ulikuwa machungoni au shambani, acha gum-boot nje, nawa miguu, toa jasho ile, mchana.

Paulo apendekeza kwamba Mst. 8-9

8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

Oa au uolewe na usisahau kupalilia uhusiano wako na mpenzi wako. Ni muhimu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!