Maelekezo Ya Ndoa

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Maelekezo Ya Ndoa
/
I Wakorintho 7:25-40

Hujambo msikilizaji wangu mahali popote ulipo. Leo twalichambua fungu la Neno kutoka 1 Wakor.7:25-40. ‘MAELEKEZO YA NDOA.’ Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Karibu tena, tulichambue Neno kutoka 1 Wakorintho 7:25-40. Maelekezo ya ndoa. Ndoa ni uhusiano wa kudumu, tena wa karibu. Bibilia husema, katika Mwanzo 2:23-24

23 Adamu akasema sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, basi ataitwa mwanamke.

24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja.

Bwana wetu Yesu kristo, aliueweka ukweli huo, mhuri. Nasoma, Injili ya Marko 10: 6-12

6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.

7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye ataambatana na mkewe

8 na hao waili watakuwa mwili mmoja, hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

9 Basi alichounganisha Mungu mwanadamu asitenganishe.

10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.

11 Akawaambia, kila mtu atakayemwacha mkewe na kuwa mwingine azini juu yake

12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.

Siku hizi yaonekana kwamba hatutilii maanani maagizo yake mungu katika ndoa zetu: talaka na kutokuaminika, zimekuwa habari za kila siku.

Ukifungua kurasa za magazeti yetu, utasoma mambo kama;

“Mume wangu hudhulumu binti ya dadangu kila siku.”

“Nataka mwenye pesa, yaani, Kaka ana shida ya pesa na badala ya kutafuta ajira, atafuta mwanamke mwenye pesa. Hiyo ndio sababu yake ya ndoa.”

Mambo kama hayo ni dhambi na ni makosa. Ndoa ya aina hiyo haidumu. Zaidi sana, uasherali umevunja ndoa nyingi. Acha ya kuchovya nje. Hiyo tabia huangamiza. Shimo lisilo mwisho, wahenga walisema: Usiuze huduma zako.

Neno lasema hivi katika 1 Wakorintho 7:25-40.

25 Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za bwana kuwa mwaminifu.

26 Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo

27 Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke.

28 Lakini, kama ukio huna hatia, wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao, watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

29 Lakini ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake, na wawe kama hawana.

30 na wale walio kama hawali na wale wafurahio kama hawafurahi, na wale wanunuao, kama hawana kitu.

31 Na wale watumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu, huu yanapita.

32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishighulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje bwana,

33 bali yeye aliyeoa hujishighulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakayompendeza mkewe.

34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.

35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile, vipendezevyo tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine

36 lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendevyavyo, na ikiwa huyo amepitia uzuri wa ujana wake na ikiwapo haja, basi afanye apendavyo, hatendi dhambi na awaruhusu waoane.

37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake atatenda meme.

38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye aiyemwoza tazidi kufanya vema.

39 Mwanamke hufungwa maadamu mwenye uhai, lakini ikiwa mumewe ametariki, yu huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye katika Bwana tu.

40 Lakini heri yeye azidi akikaa kama alivyo, ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi name nina roho ya Mungu.

Ndoa zetu zitafaulu hata ikiwa kuna makosa kidogo kidogo za ya kibinadamu. Zitafaulu katika BWANA, yaani, wawili hao, wakiwa wamemwamini Yesu Krsito kweli. Si kwa midomo tu. Kukiri, na kumwamini Yesu.

Pamoja na hayo, ni vizuri na vyema kupata Baraka za wazazi, katika Bwana.

Sote tukimwamini na kumtii Bwana Yesu Kristo, hatutahayarika. Bwana atazineemesha ndoa zetu.