Namna Ya Kujua Mwisho Wakaribia

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Namna Ya Kujua Mwisho Wakaribia
/
Mathayo 24:1-14

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi na wakati wa kulichambua neno la Mungu. Injili ya Mathayo 24:1-14. Hapa twazipata dalili za siku za mwisho. Jina langu ni David Mungai.

Naamini ya kwamba, mtu awaye yote mwenye akili timamu ajua ya kwamba dunia hii itafika mwisho wake. Sisi twaishi miaka sabini na ikiongezwa na mungu huwa miaka ya shida. Biblia yatuonyesha mwanzo n ahata mwisho. Watu wengine wamejaribu kutoa hesabu zao za mwisho wa dunia lakini wakosea ni mung utu anayeweza kuleta mwisho wa dunia na kwa wakati unaofaa. Mungu muumba wa mbingu nan chi ndiye tu anayo mamlaka ya kufanya apengavyo na viumbe vyake na kwa wakati unaofaa, na yote twayapata katika neno lake. Yesu Kristo ajua ya mwisho, maana aliwaonyesha wanafunzi wake kama tunavyosoma kutoka Mathayo 24:1-14. Nasoma Injili ya Mathayo 24: 1-14

Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, hamyaoni haya yote? Amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema, tuambie mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako nay a mwisho wa dunia? Yesu akajibu akawaambia angalieni mtu asiwadanganye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo nao watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita, angalieni, msitishwe maana hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.

Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa na ufalme kupigana na ufalme kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki nao watawaua, nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Hakika Yesu alijua dalili ambazo zaonyesha mwisho au siku za mwisho zakaribia. Tuziangalie tuzichunguze hizo dalili kwa undani Zaidi. Maslahi ya waliomwishi wanafunzi na mitume wa Yesu, yataonyesha dalili Fulani siku za mwisho zikikaribia. Labda wanafunzi wa Yesu walitamani ile hekalu iliyokuwa Yerusalemu wakautamani umaridadi na mjengo wa lile hekalu. Mfalme Herodi aliijenga ile hekalu kwa ustadi sana, ilijengwa kwa dhahabu na mawe ya aina mbalimbali, yakangarisha kweli. Ndipo Yesu akawashangaza wanafunzi wake kwa kusema “Amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.”

Herode alianza kujenga lile jingo la hekalu mnamo mwaka wa 20 BC. Na lile jingo lilimalizika mnamo mwaka wa AD 64. Lile jingo lilijengwa na mawe yaliyokuwa kati ya pili 10 hadi kumi na mbili kwa urefu na yalionekana wazi, hata wa leo, yametapakaa lilipokuwa lile jingo baada ya kuharibiwa mnamo mwaka wa A.D 70, na wanajeshi wa kirumi.

Wanafunzi wakamuongoza Yesu, wakapita bonde la kedroni walipofika mlimani wa mizeituni wakatazama nyumba na wanafunzi wakamwomba Yesu awaambie mambo yale yatafanyika lini. Alijibu akawaambia

  1. Ninyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni msitishwe maana hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
  2. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Yetu ni kusikiliza na kutizama kwa makini.
  3. Yesu alisema “wengi watakuja kwa jina langu wakisema, mimi ni Kristo, nao watadanganya wengi.” Halafu Yesu