Je Yesu Atarudi Na Nguvu – Part 1

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Je Yesu Atarudi Na Nguvu - Part 1
Loading
/
Mathayo 24:15-28

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha kujifunza neno la mungu. Twalitazama kwa undani fungu la neno kutoka Injili ya mathayo 24:15-28. Je, Yesu Kristo atarudi kw anguvu au mamlaka ya aina gani. Jina langu ni David Mungai.

Hakika tunajua ya kwamba ulimwengu upo katika hali mbaya sana. Watu wengi sana watafuta ukombozi. Je, mambo yatabadilika kuwa mema? Yesu aliwaambia mitume wake kwamba mambo nchini yataendelea kuwa mabaya. Yesu akafundisha mitume. Mat 24:15-28

“Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel limesimama katika patakatifu, asomaye na afahamu. Ndipo walio katika uyahudi na wakimbilie milimani, naye aliye juu ya dani asihuke kuuichukua mwake, wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwako dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupishwa asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupishwa siku hizo. Wakati huo mtu akiwaambia, tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza kama yamkini hata walio wateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani, msitoke yumo nyumbani msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu. Kwa kuwa po pote ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai.”

Kutoka kwa fungu hili la neno la mungu, nayaona masomo maalum ambayo ni muhimu kuyaelewa. Chukizo. Yesu alisema katika mstari wa 15, basi hapo mtakaloliona chukizo la unaribifu lile lililonenea katika patakatifu asomaye na afahamu. Swali ni hili: chukizo hilo alilonena Danieli ni lipi? Basi lazima tusome kitabu cha Danieli 11:29-31

“Kwa wakati ulioamriwa atarudi na kuingia upande wa kusini lakini wakati wa mwisho hayatakuwa kama yalivyokuwa wakati wa kwanza. Maana merikebu za kitimu zitakuja kupigana naye, basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhibika hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo naam, atarudi na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.

Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku nao watasimamisha chukizo la uharibifu.”

Yesu alipozungumza na mitume wake kuhusu lile chukizo alizungumzia unabii wa danieli wakati dhabihu za kila siku zingekomeshwa, na mahala pake pawekwe dhabahu la sanamu. Kunako mwaka wa AD 70, warumi waliharibu hekalu la Yerusalemu. Hilo ni chukizo machoni mwa mungu.

Imetendeka yawezekana itatendeka tena, na ikitendeka tena wale waliopo udea wakimbilie milimani. DHIKI: Yesu ataka kila mmoja kujua ya kwamba mambo yatafanyika haraka na kwa upesi kasi sana. “naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake. Wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.” Litakuwa jambo la haraka na upesi bila kurudi nyuma. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo. Itakuwa mateso na dhiki, na waombe isiwe siku ya sabato. Mstari wa 21. “kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”

Wakati wa kuharibiwa hekalu mnamo AD 70, wayahudi waliteseka sana. Zaidi ya millioni moja walichunjwa na jeshi la kurumi. Lakini Bwana Yesu akasema ya kwamba kutakuwa na wakati wa dhiki kuu, siku zijazo na siku za dhiki kuu zitafupishwa la sivyo hakuna mtu atabaki lakini kwa ajili ya wateule zitafupishwa.

Makristo wa uongo. Mst 23 wakati huo mtu akiwaambia, tazama kristo yupo hapa au yuko kule. Msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo na wataloa ishara kubwa za maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.

Tujihadhali na watu kama hao wala tusiwafuate. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.

Sifa ni kwake mungu, maana kristo yu arudi kutunyakua. Mungu tusaidie kuondoa vikwazo vyote vywa dhambi kutubu na kuungama na kimwili Yesu kristo kuwa mwokozi na mkombozi wetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!