Vile Ulivyo Waguza Wengi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Vile Ulivyo Waguza Wengi
Loading
/
Mathayo 23:1-12

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha kujifunza Neno la mungu la Matumaini. Leo twajifunza namna ya kuwaguza watu wengine mahali mungu ametuweka. Jina langu ni David Mungai.

Nyakati ni nyingi tunasema Fulani ndiye aliyenivutia kufanya au kuwa mahali Fulani. Mahali ulipona unapofanya mambo yako, watu wakisoma Je waandika barua ya aina gani? Namna unavyozungumza waweza kuwaleta watu karibu au kuwapotosha. Na je, maneno na matendo yako yakubaliana? Ni changamoto kweli. Pia ilikuwa changamoto kwa mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Nasoma kutoka Injili ya Mathayo 23:1-12.

Kisha Yesu akawambia makutano na wanafunzi wake akasema, waandishi na mafarisayo wameketi katika kiti cha Musabasi yo yote watakayowaambia myashike na kuyatenda lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende, maana wao hunena lakini hawatendi.

Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao, wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu, kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao, hupenda viti vya mbele katika karamu na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni na kuitwa na watu Rabi, bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja nanyi wote ni ndugu.

Wala msimwite mtu baba duniani, maana baba yenu ni mmoja aliye wa mbimguni. Wala msiitwe viongozi maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza atadhiliwa, na ye yote atakayejidhili atakwezwa.

Yesu alizungumza na watu na mitume wake kuhusu mafarisayo waliokuwa waalimu. Yesu alisema kwamba waliketi kwa kiti cha musa, kwa kifupi ni kwamba waliamini na kufundisha neno la mungu na msingi wa mafundisho yao ulikuwa neno la mungu na twajua neno la mungu ni kweli. S Mafundisho ya kweli na ukweli kina chake huwa neno la mungu. Sharia ya mungu na torati walifundisha watu wote. Ni muhimu kuyazingatia yaliyo ndani ya neno la mungu lililohai. Walivuta watu kwao maana walifundisha neno la mungu. Ukifundisha ukweli wa neno la mungu, utawasaidia na kuwavuta wengi kwake Yesu Kristo. Mafarisayo walifundisha katika hekalu na masinagogi. Mawazo yao yalikuwa ya kipekee, kanzu ndefu na safi nayo pia iliwavutia wengi lakini nyakati zingine walikuwa wafisadi.

Twaweza kufundisha ukweli wa neno. Twaweza kuvaa nguo za heshima, lakini matendo naomba yasiwe na ufisadi. Tusiwe watu wa kukata kona kona. Tabia maneno, na matendo lazima ziende sambamba. Ukweli mwingine ni lazima tujifunze kuchukuliana mizigo na kuwa na ushirika n akuombeana na hivi tutawavuta wengi kwake mwokozi wetu Yesu Kristo. Mwandishi wa waraka kwa waebrania aliwakumbusha hayo kwa maneno haya.

Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, usigeuke maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu tuangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri, wala tusiache kukusanyika pamoja kama iliyo desturi yaw engine bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Yaani tuwe waungwana kiasi tunapofanya hivyo uhusiano wetu na ushirika kama wakristo ni muhimu na huwavuta wengi kwetu na kwa kristo. Tuwe wanyenyekevu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!