Watu Wema Wanaposea

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Watu Wema Wanaposea
Loading
/
Mathayo 23:13-22

Hujambo n akaribu. Leo katika tumaini twalichambua neno kutoka Injili ya mathayo 23:13-22 “Watu wema pia hukosea.” Jina langu ni David Mungai.

Siyo watu wengi hupanga kufanya makossa. Lakini twakosea kila wakati. Hayo twajua. Lakini lazima tujue na tufahamu ya kwamba, ni kwa nguvu za mwenyezi mungu twaweza kuacha kuwa na tabia ya kukosea kila wakati. Ni vyema kujua ya kwamba hukuna tunaloweza kufanya bila kuwezeshwa na mwenyezi mungu. Hebu nisome Injili ya Mathayo 23:13-22. Yesu alisema maneno makali:

“Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni, ninyi wenyewe hamwingii wala wanaoingia hamwaachi waimgie. Ole wenu waandishi kwa kuwa mnakula nyumba za wajane na kwa unafiki mnasali sala ndefu kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa Zaidi. Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki kwa kuwa mnazunguka katika bahari nan chi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu na akiisha kufanyika mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili Zaidi kuliko ninyi wenyewe. Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao mtu atakayeapa kwa hekalu si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu amejifunga. Wapumbavu ninyi na vipofu maana ni ipi iliyo kubwa ile dhahabu au lile hekalu liitakasalo dhahabu? Tena mtu atakayeapa kwa madhabahu si kitu bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake amejifunga. Vipofu ninyi maana ni ipi iliyo kubwa ile sadaka au ile madhabahu litakasayo sadaka?

Basi yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. Naye aapaye kwa hekalu huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake. Naye aapaye kwa mbingu huapa kwa kiti cha enzi cha mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.”

Kutoka kwa fungu hili la neno la mungu, Yesu atufunulia matokeo kwa watu ambao hukosea kama sisi. Jambo la kwanza ni kuwa bidi yao ya kufanya makossa huwa kikwazo kwa wale wangeingia mbinguni. Pampja na hayo huwapotoza wengi wanapowatendea na wajane maovu kwa jina la maombi. Sikiliza maneno ya Yesu. “Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane na kwa unafiki mnasali sala ndefu kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa Zaidi” Ni kilio na hukumu kwa wanaopotoza wajane maovu. Wamehukumiwa na hukumu iliyo kubwa Zaidi. Pia ni kilio kwa wale wanaowaleta watu kwa Imani halafu huwekelea mizigo mingine mizito wasioweza kubeba. Kama wafanya hivyo, acha na utubu maana neno limesema ya kwamba utapata hukumu iliyo kubwa Zaidi.

Wengine ambao watapata hukumu kubwa ni wale ambao huapa hata kwa jina la mungu, hali wajua wasema uongo. Kumbuka ya kwamba mungu ajua ukweli wote nay eye mwenyewe ndio kweli inayodumu. Yesu alisema “mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi” Huwezi kumndanganya mungu na anajua ukweli wote. Acha kuapa kwa jina la mungu, hali unajua wasema uongo, au nusu uongo, maana utapata hukumu kubwa. Ni kama kukufuru bwana. Pia watalia wale wanaoleta utani katika mambo ya muhimu ya torati na sharia. Ms wa 23: “Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnaa na bizari na jira lakini mmeacha mambo makuu ya sharia, yaani adili na rehema na Imani, hayo imewapasa kuyafanya wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”

Yaani mafarisayo na waandishi waliangalia mambo madogo madogo na kuyaacha yaliyo ya maana na muhimu. Walifanya hivyo makusudi na kwa faida yao wenyewe.

Bidi zai, ni kwa manufaa yao wenyewe sio kwa kanisa ay kwa utukufu wa mungu. Ni dhambi na ni makossa. Heri atakayetubu na kuungama hiyo dhambi na ajiunge na wenye haki na kweli.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!