hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mwisho
Loading
/
Danieli 8:15-27

Hujambo na karibu tujifunze Neno pamoja. Danieli 8:15-27. “MWISHO” Jina langu ni David Mungai Yesu ni Bwana. Wimbo halafu tuendelee mbelee.

Naam. Karibu tena. Twalichambua Neno kutoka kitabu cha Danieli 8:15-27.

Nasoma 15 Ikawa mimi, naam, mimi Danielii, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.

16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.

17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.

18 Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.

19 Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.

20 Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.

21 Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.

22 Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.

23 Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.

24 Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.

25 Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.

26 Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi.

27 Na mimi, Danielii, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.

Kutoka kwa lungu hili la Neno la Mungu, twamwona Gabrieli mjumbe wa mwenyezi Mungu (mst 16-17), kwamba ujunbe huu, katika lungu hili la Neno litatimilika katika siku za mwisho ulioamrishwa.

Na kwa wakati huo huo, mjumbe Gabrieli akamwonyesha Danieli kondoo mwenye pembe mbili zasimmia falme mbili, ufalme wa Pashia na Media. Na beberu mkubwa asimamia utawala wa Kiyunani/Kigiriki.

Kuanzia mstari wa 23-26, Fungu hili latazamia siku zijazo, wakati mpinga Kristo ataonekana wazi wakati wa dhiki. Siku hizi twaona roho za wapinga Kristo wengi kwa mafundisho na mahubiri lakini kunao wakali katioka historia ambao nguvu za shetani na mpinga Kristo zitaonekana wazi. Atatenda makuu na hata miujiza kwa utukufu wake mwenyewe kinyume ya miujiza aliyotenda Kristo kwa utukufu wa Mungu Baba.

Lakini kulingana na kufuatana na mafunzo ya kitabu cha Ufunuo (19:11-16, 18-21, 20-10) Mungu atamshinda Yule mpinga Kristo katika vita vikuu vya Armegeddoni.

Katika mstari wa 26-27 Danieli alishangazwa na maono hayo, ingawaje alikuwa nabii hakuelewa. Lakini ilibidi akubali kwa sababu mjumbe wa mwenyezi Mungu amesema.

Danieli alionyeshwa mateso ya watu wa taifa lake Israeli akahuzunika mno. Hata hivyo, mjumbe wa Mungu akamwambia katika mstari wa 26-27.

26 Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi.

27 Na mimi, Danielii, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.

Hata nasi bado twangojea kwa hamu, baada ya kunyakuliwa kwa kanisa, mateso ya dhiki kuu yataanza humu duniani, kwa wayahudi kwanza na watu wa mataifa . Njia kuepuka dhiki kitu ni kumwamini Yesu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!