Matakwa Yake Mpinga Kristo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Matakwa Yake Mpinga Kristo
Loading
/
Danieli 11:30-45

Hujambo na karibu leo katika matumaini. Twalichambua fungu la Neno linalomhusu ‘mpinga Kristo’ atakayekuweko wakati wa miaka saba ya dhiki Danieli 11:30-45. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena tujifunze neno pamoja. Danieli 11:30-45

30 Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhabikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.

31 Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.

32 Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.

33 Na hao walio wenye hekima katika watu watafundisha wengi; hata hivyo wataanguka kwa upanga, na kwa moto, na kwa kufungwa, na kwa kutekwa nyara, siku nyingi.

34 Basi watakapoanguka, watasaidiwa kwa msaada kidogo; lakini wengi wataambatana nao kwa maneno ya kujipendekeza.

35 Na baadhi yao wenye hekima wataanguka, ili kuwatakasa, na kuwasafisha, na kuwafanya weupe, hata wakati wa mwisho; kwa maana ni kwa wakati ulioamriwa, ambao haujaja.

36 Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu,naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika.

37 Wala hataijali miungu ya baba zake; wala yeye aliyetamaniwa na wanawake; wala hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya wote.

38 Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo.

39 Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; nay eye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa,

40 na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.

41 Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, nan chi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni.

42 Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka.

43 Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.

44 Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha, naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi.

45 Naye ataweka hema zek za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.

Katika mstari wa 21, katika surah ii, twapata maneno yanayotuonyesha ya kwamba, kutotea mtu wa kujipendekeza, yaani atatawala kwa kujipendekeza na afananishwa na mmoja aliyeitwa Antiochus Epiphanes, atakayepatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, na kuondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watasimamisha chukizo la uharibifu.

Antiokia, aliyatia madhabau unajisi, alipomtoa nguruwe dhabihu juu ya madhabau mnamo mwaka wa 168 BC

Na jambo kama hilo litafanyika tena wakati wa ule wakati wa dhiki wakati ambapo mpinga Kristo, atakapotia unajisi hekalu mjini Yerusalemu atakapotaka kwa lazima aabudiwe na kutukuzwa kuwa Mungu kama tunavyosoma katika mstari wa 36. Naye mfalme atafanya kama apendavyo…

Mstari wa 40, waonyesha kwamba, hatakuwa mfalme wa kaskazini-yaani(Asuli), wala hatatoka kusini – (misri), lakini ni wazi kwamba mambo yatatendeka wakati ujao kama alivyoeleza Bwana wetu Yesu Kristo katika injili ya Mathayo 24:15

“Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).”

Katika mstari wa 45, fungu la Danieli 11, laonyesha ya kwamba, mpinga Kristo ataendelea kujivuna, kujiinua kuliko wengine wote kama Mungu, mpaka, ule wa wakati wa kuondolewa na nguvu za Kristo, kama tunavyosoma maneno ya mstari wa 45.

“Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri, lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.”

Katika mstari 37-38, twapata maneno haya “…wala yeye aliyetamaniwa na wanawake…” Baadhi ya walimu wa Bibilia wamesema ya kwamba mpinga Kristo atakuwa soga yaani hataoa. Bado walimu wengine wasema ya kwamba mpinga Kristo, hatawajali wanawake wa Wayahudi na kuwaheshimu kama mama na masihi.

Kwa kifupi ni kusema, mpinga Kristo hatayajali mafundisho na matendo ya Mungu na Neno lake. Na mstari 40-41 twapata maneno haya “…na wakati wa mwisho…mpinga Kristo na majeshi yake kutoka kaskazini na kusini na majeshi mengi kutoka nchi nyingi, watakusanyika katika vita vya Armageddon kuangamiza Israeli, na wakati huo huo, Bwana wetu Yesu Kristo atashuka na majeshi yake ya malaika wakiongozwa na malaika Mikaeli, na kuyashinda majeshi ya mpinga Kristo.

Mpinga Kristo atawekwa kuzimu kwa miaka elfu moja, wakati wa utawala wake Kristo, kisha atafunguliwa kidogo na kuhukumiwa hukumu ya mwisho katika bahari ya moto. Baada ya hayo, Wakristo tutaishi na Yesu Kristo, milele na milele. Ufunio 19:11-21

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!