Mungu Ndiye Hugawa (Mpaka)

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ndiye Hugawa (Mpaka)
Loading
/
Warumi 9:6-13

Hujambo. Jina langu ni David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi cha Matumaini. Katika kipindi hiki sisi hulichambua neno na yeyote anayetusikiliza. Leo twalichambua fungu kutoka Waraka wa Paulo kwa Warumi 9:6-13 “MUNGU NDIYE HUGAWA” Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam karibu tena tujifunze pamoja Warumi 9: 6-13. Nasoma.

“Sisemi kwamba ahadi ya Mungu imebatilika; maana si watu wote wa Israeli ni wateule wa Mungu.

7 Wala si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazawa wake watatokana na Isaka.”

8 Ndiyo kusema, si wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.

Mungu husema neno lililo na uhakika. Neno la kusadikika, Neno la ahadi. Amesema mst “…watoto wa ile ahadi wamehesabiwa kuwa wazao.” Mtoto wa ahadi amekuwa mzao atakayeridhi ya baba. Mtoto wa baba ndiye mrithi. Asiyekuwa wa baba si mrithi. Pana mpaka wazi. Mtu akizaliwa upya kwa kumwamini Yesu, Mungu humfanya yule mtoto mwana wa urithi wa uzima wa milele.

Msingi mwingine ni kwamba ahadi za Mungu ni kweli maana yeye ndiye kweli katika Yesu Kristo. Mungu akitoa neno , tayari lile neno limekamilika , haijalishi hali ya mazingira. Katika mstari wa 17 twapata kutimizwa kwa yale yaliyotabiriwa katika kitabu cha mwanzo 17.

Ibrahimu na Sara walipokuwa wakongwe walipata kijana mwanaume Isaka.

9 Maana ahadi yenyewe ni hii: “Wakati maalumu nitarudi, naye Sara atapata mtoto.”

10 Tena si hayo tu, ila pia Rebeka naye alipata mapacha kwa baba mmoja, yaani Isaka, babu yetu.

11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,

12 Rebeka aliambiwa kwamba yule mtoto wa kwanza atamtumikia yule wa nyuma. Hivyo uchaguzi wa Mungu unategemea jinsi anavyoita mwenyewe, na si matendo ya binadamu.

13 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.”

Kutoka kwa fungu hili la neno la Mungu, twapata misingi kadhaa ambayo Mungu huonyesha mipaka. Maneno ya mstari wa sifa yaonyesha kwamba Mungu hasemi maneno yasiyo na maana. Na kutoka kwa uzao wa Isaka, Yesu alizaliwa kama ilivyotabiriwa akawa ndiye Mwokozi Yesu- Immanueli, Mungu pamoja nasi. Mkombozi wetu. Ahadi za Mungu ni msingi timamu usiyotingizika.

Msingi wa tatu: Ahadi zake Mungu huleta tumaini la kutegemewa. Isaka pia alimlilia Mungu naye Mungu akalifanikisha neno lake. Isaka alimlilia Mungu afunue tumbo la mkewe Rebeka . Mungu kwa uaminifu wake, Rebeka aliifunguavijana wawili, Esau na Yakobo kama tunavyosoma katika mstari wa 11 na 12. Warumi 9: 11-12

(Kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto wala hawajatenda neno jema ala baya ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua si kwa sababu ya nia yake aitaye) 12 aliambiwa hivi mkubwa atamtumikia mdogo. Na watoto hao wawili walimalizia na kuwa mtoto wa kwa za (Esau) alimtumikia wa pili (Yakobo).

Mungu huyagawa mabo yake kulingana na vile amesema katika neno lake na kulingana na ahadi zake na kusudi lake. Basi tuyatilie maanani anayosema Mungu ahadi zake , na makusudi yake ; Neno la Bwana halitamrudia bure. Na huo ndio ukweli.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!