Mgogoro Na Dhambi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mgogoro Na Dhambi
Loading
/
Warumi 7:15-25

Hujambo na karibu, leo twalichambua fungu la neno la mungu, warumi 7:15-25, mgogoro na dhambi. Jina langu ni david mungai, wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Karibu tena. Kila mmoja wetu ajua ya kwamba kunao mgogoro, mvurutano kati yaw ema na mabaya, kati ya tamaa za kimwili na Maisha ya kiroho. Twa tamani kutenda mema lakini mwisho mwisho wa mambo sisi hutenda mabaya. Kwanini huo mgogoro, nasoma kutoka waraka wa Paulo kwa waroma, 7:15-21

15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.

17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.

Katika fungu hili twapata mabo kadhaa ya busara kuhusu mvurugano wa dhambi ndani yetu. Shina na mizizi ya dhambi imo ndani yetu Paulo amesema

15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

Ni vita ndani yetu. Twajua yale mema kutenda lakini sisi hutenda kinyume

Utu wa ndani hufuahia kutii sheria na torati lakini mwili hutenda kinyume

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.

Maneno haya yanatupatia tumaini tumshukuru mungu kwa yesu kristo bwana maana kwa kumwamini twakamilisha matakwa yote ya sheria na Imani katika kristo hutukomboa nahukumu ya sheria ambayo ni mauti ya milele tuna ukombozi katika kristo vita ipo lakini tuna ushindi katika kristo

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!