Furaha Katika Tumaini

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Furaha Katika Tumaini
/
Warumi 5:1-5

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha matumaini na katika kipindi hiki sisi hulichambua neno. Leo twalichambua neno kutoka kitabu cha Warumi 5:1-5 furaha katika tumaini. Jina langu ni david mungai, wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena tulichambue pamoja. Asante kwa kuniruhusu niseme pamoja nawe katika radio yako.

Msikilizaji tunapoona yale yanayotendeka katika mazingira yetu twashangaa n ahata kuhuzunika. Chuki kati ya watu n ahata mataifa. Matusi na maneno yasiyo na maana mambo yanayopaswa kuwa siri siku hizi huanikwa wazi. Lakini katika fungu hili la neno , Paulo atukumbusha kwamba twaweza kufurahi katika matumaini. Siku moja mateso na msumbuko yatafika kikomo. Nasoma kutoka walaka wa Paulo kwa Warumi 5:1-5

1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.

3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;

4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;

5 na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.

Mtume Paulo atuongoza kujua ya kwamba twaweza kufukia tumaini la utukufu katika Imani yetu kwa kufikia viwango flani

Kuingia kwa neema yake mungu maana ndiye mwenye uweza twamwamini na kumtegemea mungu sisi uweza hutoke kwake mungu katika yesu kristo ndiye na ndicho kiwango cha kwanza mst 1

1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo

Huu ni ukweli wa ajabu kwamba kwa Imani katika yesu kristo mungu baba muumba wa mbingu nan chi hutuhesabia haki. Ni furaha kujua kwa hakika tumehesabiwa haki. Naweza kufurahia katika fadhaa zangu duniani humu

Ki9wango cha pili ni twafurahia katika dhiki maana kazi yake huleta uthibiti saburi huleta uthibiti wa moyo yaan hata jambo likiwa ngumu tumaini katika kristo maana ndiye mweza wa ,a,bo yote maana pendo lake mungu kwa nguvu na uweza war oho mtakatifu. Pendo lake limemiminwa kwetu sharti na lazima tujue kwamba ulimwenguni tunayo majaribu lakitin katika majaribu mungu hutupatia nafasi au fursa ya kumwamini na kumkabidhi fadhaa zetu zote. Yeye ndiye kimbilio letu

Yesu mwenyewe alisema katika injili ya yohana 16:33

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na Amani ndani yangu ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeshuhudia ulimwengu

Majaribu tunayoyapitia maishani huleta matumaini tukifurahi kipawa cha roho mtakatifu aletaye tumaini moyoni mwetu n ahata kipawa cha tumaini kwa upendo wake mungu maneno ya mstari wa tano yathibitisha ukweli huo.

Na tumaini halitahayarishi kwa maana pendo la mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na roho mtakatifu tuliyepwea sisi.

Mungu metuahidi kwamba twapumzika katika na lwa uweza war oho mtakatifu mfariji na mwalimu wetu. Na kufurahia tumaini tulilonalo la uzima wa milele maana mungu amelikamilisha katika yesu kristo uwe na tumaini hili la uzima wa milele