Mpango Wa Mungu Wa Hali Ya Juu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mpango Wa Mungu Wa Hali Ya Juu
Loading
/
I Wakorintho 1:26-31

Natumai u huheri wa afya siku yaleo. Karibu tujifunze neno la Mungu pamoja. Leo twalitazama neno kutoka 1 Wakor. 1:26-31. “Mpango wa Mungu – maalum.”

Jina langu ni David Mungai wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam Karibu tena.Twalichambua Neno kutoka 1 Wakor. 1:26-31.

Unajisi wote hutoka ndani ya mtu, alivyosema Yesu Kristo, kutoka Injili ya Marko 7:15.

15 Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.

Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.

Ndani ya mtu hutoka uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, vitina, varaka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo… watu watendao mambo hayo hawatarithi ufalme wa Mungu.

Hata hivyo, Mungu ametupangia mpango maalum. Nasoma kutoka 1 Wakor 1:26-31.

26 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

27 Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

28 Tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;

29 Mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.

30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

31 kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

JER 9:23

Maneno haya pia yaweza patikana katika kitabu cha Nabii Yeremiah 9:23-24.

23 Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

24 bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana.”

Mambo ya Mungu ni ya ajabu na ndiyo pekee ya kutegemewa. Na mambo ya Mungu hutegemea neema yake kwetu. Si kwa nguvu zetu, au elimu, na kuhitimu kwetu ba li ni kwa uwezo na neema yake Mungu twapata wokovu kwa kumwamini yesu.

Twaitaji kuoshwa kutoka ndani, mioyo na nadhiri zetu. Twaoshwa kwa damu yake yesu na Neno lake Mungu. Tuwe na uzoefu wa kutubu na kuungama dhambi maana Mungu ametuahidi kutuosha na udhalimu wote. Maneno ya Wakor. 27-29.

27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;

29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.”
Paulo, pia, alipowaandikia Wafilipi barua hakusahau kuwaambia maneno haya.

Wafilipi 3:7-11

7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.

8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;

9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;

10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.

Paulo awaambia Wakorintho na Wafilipi pia aliyehesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu.

Kumjua Kristo na uzuri wake, hakuna cha kufanana naye. Ni uzuri usio kiasi na huleta utukufu kwa Mungu. Katika mpango wa Mungu unyenyekevu na kutubu na kumwamini Kristo ndiyo njia ya pekee ya wokovu. Na huo ndoyo mpango wa Mungu maalum. Katika Kristo, twaokolewa na kukombolewa. Yesu bado aita. Kwa imani umpokee.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!